Mzee wa 'Always next time' akabidhiwa Ngorongoro Heroes

Mzee wa 'Always next time' akabidhiwa Ngorongoro Heroes

14 Mar 2018, 12:18

Shirikisho la soka nchini (TFF) limemteua aliyekuwa kocha mkuu wa Kilimanjaro stars Ammy Conrad Ninje kuwa kocha wa muda wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes).

Ninje akiliongoza kikosi cha Kilimanjaro Stars katika michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) iliyomalizika mwishoni mwa mwaka jana nchini Kenya na kufanya vibaya kwa kushika mkia katika kundi lake bila kushinda mchezo wowote. 

Kibarua cha kwanza 

Kibarua cha kwanza cha kocha Ninje kitakuwa ni katika michezo miwili ya kirafiki ambapo Ngorongoro Heroes inatarajiwa kucheza dhidi ya Morocco na Msumbuji.

Chini ya kocha Ninje Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana Msumbiji Jumatano Machi 21, 2018 michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Michezo hiyo ni kwa ajili maandalizi ya kuwavaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana (AFCON U20) itakayofanyika mwakani nchini Niger.

Ninje ametangazwa leo katika mkutano wa wanahabari katika makao makuu ya TFF Nchini Tanzania.

Related news
related/article
International News
Former Germany captain backs coach after loss to Mexico
52 minutes ago
International News
Neymar downplays his €222m price tag
14 Jun 2018, 18:35
International News
Pepe: It's a privilege to have Ronaldo
2 hours ago
International News
Another record! Second World Cup's quickest red card
18 hours ago
FIFA World Cup
Preview: Poland vs. Senegal - Prediction, team news and lineups
21 hours ago