Ndanda v Yanga: Rostand, Kessy waanza, Gadiel kumsubiri Mngwali

Ndanda v Yanga: Rostand, Kessy waanza, Gadiel kumsubiri Mngwali

28 Feb 2018, 12:51

Kipa mkameruni Youthe Rostand amerejea kwenye majukumu yake ya kuwatumikia mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Dar Young Africans,  katika mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

Youthe Rostand ambaye hakudaka mechi yoyote ya ligi toka alipoumia katika mchezo dhidi ya Lipuli amechaguliwa na kocha George Lwandamina kuanza baada kuonesha kiwango kizuri katika mchezo wa FA dhidi ya Majimaji mwishoni mwa juma lililopita.

Rostand atalindwa na Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani na Juma Makapu katika safu ya ulinzi. Aidha huu utakuwa mchezo wa pili mfulululizo kwa Yanga kumkosa mfungaji anayeongoza kwa mabao mengi klabuni hapo msimu huu Mzambia Obrey Chirwa kutokana na Majeraha. 

Kinachoanza: Youthe Rostand, Hassani Ramadhan Hamis 'Kessy', Mwinyi Haji, Juma Saidi Makapu, Kelvin Yondani, Pato Ngonyani, Emmanuel Martin, Papy Kabamba Tshishimbi , Pius Buswita, Raphael Daud, Ibrahim Ajibu.

Benchi: Ramadhani Kabwili, Juma Abul, Gadiel Michael, Buruan Yahya, Makka Edward, Yusuph Mhilu, Geofrey Mwaishiuya.

Yanga watajitupa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara kucheza na wanakuchele Ndanda FC katika mchezo wa mwisho wa raundi 19 jioni hii.

Kufungwa kwa Yanga ama kushinda hakutabadilisha msimamo wa ligi hasa katika nafasi tano za juu ambapo Simba wanaongoza wakiwa na alama 45 huku Yanga wakiwa na alama 37.

Related news
related/article
Transfer News
Homeboyz manager opens up on Wafula exit
13 hours ago
International News
Van Gaal to blame for United struggles, Neville claims
15 Aug 2018, 13:25
Transfer News
Former Real Madrid coach linked with Man Utd
15 Aug 2018, 09:25
International News
England rise in latest FIFA rankings
19 hours ago
Transfer News
Marseille back for Chelsea forward
15 Aug 2018, 08:45