Singida United kuifuata Kagera Sugar jogoo la kwanza Alhamis

Singida United kuifuata Kagera Sugar jogoo la kwanza Alhamis

14 Feb, 12:11

Kikosi cha timu ya soka ya Singida United 'Simba wa bonde la Ufa' kinatarajiwa kuondoka mapema asubuhi ya Alhamis, Februari 15 kuelekea mkoani Kagera tayari kwa mchezo wao dhidi ya Wanankurukumbi Kagera Sugar.

Singida United ambao walipoteza mchezo uliopita dhidi ya Singida United, watakuwa na kibarua kizito watakapocheza na Kagera Sugar ambao wamekuwa na matokeo mabovu toka kuanza kwa msimu.

Akizungumza na mtandao bora wa michezo Afrika 'Futaa.com' meneja wa kikosi cha Singida United Ibrahim Ahmed amesema kikosi kimejipanga vizuri licha ya kufahamu kuwa mchezo huo hautakuwa mrahisi.

"Tumepoteza mchezo wetu wa nyumbani hivyo lazima tujipange kwa mchezo wetu unaofuata, tunajua mchezo hautakuwa mrahisi na tunajua tunakazi kubwa sana katika michezo iliyosalia," amesema Ibrahim.

Majeruhi ni kikwazo 

Aidha kikosi hicho kinaelekea Bukoba kikiwa bado na majeruhi wachache ambao kwa mujibu wa meneja Ibrahim, majeruhi hao ndio wamechangia kupoteza mchezo wao dhidi ya Stand United.

"Kikosi chetu kuwa na majeruhi wa hapa na pale kumechangia kuwa na matokeo haya ya kusuasua, ila Kwa sasa hivi majeruhi wamepungua isipokuwa kwa kipa wetu Manyika Jr ambaye anauguza goti, lakini mwalimu bado anaimani na kikosi chake ya kuwa tunanafasi ya kufanya vizuri," amesema.

Mechi ya Kagera Sugar na Singida United itafanyika Februari 17 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera ukiwa ni mchezo wa raundi ya 19 mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Related news
related/article
Local News
Sserunkuma flogs Express as Vipers edge closer to glory
22 May, 20:00
International News
Arsenal fined
22 May, 15:40
International News
Arsenal refuses to comment on new manager talk
22 May, 07:20
International News
Arsenal fined
22 May, 15:40
Transfer News
Transfer Talk: No offers from Chelsea or Zenit for Sarri
22 May, 09:10