Simba yapata pigo, kuelekea mechi dhidi ya Mwadui

Simba yapata pigo, kuelekea mechi dhidi ya Mwadui

14 Feb, 11:33

Mlinzi kiraka wa timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Mghana Asante Kwasi atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoukosa mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC siku ya Alhamisi Februari 15.

Kwasi atakaukosa mchezo huo kwa mujibu wa kanuni za ligi baada ya kupata kadi tatu za njano katika michezo iliyopita, kama alivyothibitisha meneja wa klabu Robert Richard.

"Niseme tu Asante Kwasi tayari ana kadi tatu kwa hiyo hatotumika kwenye mchezo dhidi ya Mwadui, waliobakiwa ni wale ambao bado wanauguza majeraha yao nao hawatakuwa sehemu ya mchezo huo "Na kusema ukweli kwa ripoti ya daktari wiki ijayo kwa wachezaji majeruhi wanaweza kurejea na tukaanza nao mazoezi," Richard ameongeza.

Robert amesema wanajua fika namna ambavyo Mwadui wameimarika kwa siku za hivi karibuni, hivyo wanaendelea kujipanga kuhakikisha mapengo ya wachezaji hao yanazibwa na wanaibuka na ushindi.

Umoja na ushirikiano 

Katika hatua nyingine klabu ya Simba imewaomba mashabiki wake kuendeleza na kuimarisha ushirikiano walionao hivi sasa ili kuweza kuendelea kupata matokeo chanya.

Klabu imesema inawashukuru sana mashabiki wake kwa namna ambavyo wamejitoa mpaka sasa na kwamba waendelee Lakini moyo huo huo hata pale timu inapokuwa inapata matokeo mabaya.

Simba watamaliza raundi ya 18 wakiwa kileleni mwa ligi kwani mpaka sasa wana alama 41 ambazo hata kama wakipata matokeo mabaya dhidi ya Mwadui FC hakuna timu ambayo inaweza kuwafikia kileleni.

Matokeo mengine VPL raundi ya 18.

FT: Njombe Mji 0-0 Mbeya City

FT: Singida United 0-1 Stand United

FT: Mbao FC 0-0 Mtibwa Sugar

FT: Ruvu Shooting 3-1 Lipuli FC

FT: Ndanda FC 0-0 Tanzania Prisons

Ratiba ya raundi ya 18.

Feb 14, 2018: Dar Young Africans v Majimaji

Related news
related/article
International News
Guardiola hails new Arsenal boss
13 hours ago
International News
OFFICIAL: Arsenal release new home kit for 2018/19 season
22 May, 13:35
International News
Spain announce 23-man FIFA World Cup squad
21 May, 15:50
International News
WC 2018: Spain's World Cup rejects starting XI
22 May, 07:45
Transfer News
Transfer Talk: No offers from Chelsea or Zenit for Sarri
22 May, 09:10