Majimaji yawataka waamuzi kuwa 'fair' mchezo dhidi ya Yanga

Majimaji yawataka waamuzi kuwa 'fair' mchezo dhidi ya Yanga

14 Feb, 10:22

Timu ya Majimaji imewataka waamuzi wa mchezo dhidi yao na Mabingwa watetezi wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara Dar Young Africans kuzingatia sheria 17 pasipo kupendelea timu yoyote katika mchezo ambao utafanyika Jumatano kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na futaa.co.Tz Afisa habari wa Timu hiyo Onesmo Ndunguru amesema kuwa kama waamuzi watafuata sheria basi kila timu itakuwa na nafasi kubwa kushinda kulingana na maandalizi waliyoyafanya.

Hata hivyo Ndunguro amelalamika kuwa waamuzi wamekuwa wakiwaonea katika michezo yao na kupelekea timu hiyo kupata matokeo yasiyo ya kuridhisha. 

"Waamuzi wawe fair wasiwe wakuisaidia Yanga kushinda, wakiwa fair na sisi tutaweza kucheza na kuonesha uwezo wetu waamuzi wamekuwa wakituonea", amesema Ndunguru. 

Kuhusu maandalizi ya Timu Ndunguru amesema timu ipo vizuri na vijana wana ari na morali ya kushinda bila kuzingatia nafasi yao kwenye msimamo huo ambapo wako katika nafasi ya 14 wakiwa na alama 14. 

Timu bora ishinde

"Timu ipo vizuri vijana wana ari ya kufanya vizuri pasipo kuangalia tupo katika mazingira gani kwa sababu kwenye msimamo tuko katika nafasi ya 14 lakini hii haiwafanyi vijana kujidunisha, lakini wana amini chochote kinaweza kikatokea ni mchezo mgumu lakini ni lazima Majimaji tushinde ama tupate sare, kikubwa lazima tuwe na commitment, kwa hiyo vijana wana commitment kubwa kuelekea mchezo huo pasipo kujali Yanga wako katika nafasi gani ama Yanga wako na ukubwa gani,"

"kila mchezo unakuwa na discipline yake Yanga akiwa na discipline ndogo ataadhibiwa Majimaji akiwa na ndogo pia ataadhibiwa", amesema Ndunguru. 

Majimaji haijashinda mchezo wowote kati ya michezo mitano ya hivi majuzi wakipoteza michezo miwili na kutoka sare michezo mitatu.

Kwa upande wao Yanga SC wambao wako katika nafasi ya 3 wakiwa na alama 34 wamepata ushindi katika michezo yote minne ya hivi karibuni. 

Michezo mitano ya Majimaji iliyopita. 

Majimaji 0 - 0 Tanzania Prisons 

Majimaji 1 - 2 Mbeya City 

Simba 4- 0 Majimaji

Majimaji 1 - 1 Singida United

Majimaji 1- 1 Azam.

Related news
related/article
International News
UEFA Champions League final: Key players
15 hours ago
International News
Arsenal fined
22 May, 15:40
Local News
SC Villa title hopes end in Proline draw
21 May, 21:30
International News
Wright slams Arsenal over Emery
22 May, 11:30
International News
Real Madrid v Liverpool: Is the Champions League enough to save Zidane?
22 May, 15:10