Mohammed Fakhi: Kagera Sugar ndio kumekucha

Mohammed Fakhi: Kagera Sugar ndio kumekucha

13 Feb, 09:20

Beki wa Timu ya soka ya Kagera Sugar Mohammed Fakhi, amesema kuwa jitihada za kuimarisha nafasi yao katika msimamo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara zinaendelea kuzaa matunda na kuwa wanatarajia kuendelea kupanda juu.

Fakhi amesema kuwa licha ya msimu kuanza vibaya mambo yameanza kuwa mazuri kutokana na bidii wamekuwa wakifanya.

Mapito

"Mi nahisi ni changamoto katika ligi tunapitia Mapito lakini tunaendelea kupambana kuipeleka timu katika nafasi za juu naamini tutakaa sawa na tutaweza kuipeleka nafasi za juu kabisa," amesema.  

Kuhusu changamoto ambazo zimekuwa zikiwazuia kufanya vizuri Fakhi amesema ni mambo tu ya kawaida ya mpira na wala sio uongozi au timu kushuka kwa kiwango.

"Mimi nahisi ni hali ya mpito tu kila mmoja anapitia mwaka jana tulicheza katika kiwango kizuri safari hii tunapitia kwenye majaribu lakini naamini tutarekebisha na kufanya vizuri", amesema Fakhi.

Kagera Sugar ambao walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo ambao ulifanyika Jumatatu ya Februari 11 wanashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 14 baada ya kucheza michezo 18.

Mchezo ujao Wanakurunkumbi hao watakuwa nyumbani dhidi ya Singida United mchezo ambao utafanyika Jumamosi Februari 17, 2018 mkoani Kagera.

Related news
related/article
International News
Transfer talk: City eyes Kompany successor as Courtois delays contract talks
18 hours ago
Local News
Sserunkuma flogs Express as Vipers edge closer to glory
22 May, 20:00
International News
Cazorla leaves Arsenal
21 May, 21:17
International News
WC 2018: Spain's World Cup rejects starting XI
22 May, 07:45
International News
Buffon to decide future next week
22 May, 08:50