Ndanda wazimezea mate pointi  za Mbao

Ndanda wazimezea mate pointi za Mbao

12 Jan 2018, 17:34

Wanakuchele, timu ya soka ya Ndanda imebainisha kuwa wapo tayari kabisa kwa mchezo wa ligi dhidi ya timu ya soka ya Mbao utakaofanyika Januari 13 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Ndanda imesema kuwa wamepata muda mzuri wa maandalizi toka walipocheza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Simba na kukubali kichapo cha mabao 2-0, hivyo wanaenda katika mchezo dhidi ya Mbao wakiwa na ari kubwa ya kupata matokeo chanya.

Msemaji wa Ndanda Idrisa Bandali amesema maandalizi waliyoyafanya yanatosha kabisa kuwapa kiburi cha kusema kuwa wataibuka na ushindi ili kumaliza kiu ya mashabiki wake kuona timu yao inapata pointi tatu wakiwa uwanja wa nyumbani.

-Kikubwa ambacho tunamshukuru Mungu ni kuwa mpaka tunakamilisha mazoezi yetu, hakuna taarifa yoyote ya mchezaji kuwa na tatizo la kiafya, maana yake wachezaji wote ni wazima, tunataka kushinda kwani ni muda mrefu hatujashinda katika uwanja wetu wa nyumbani, mara ya mwisho nakumbuka tuliwafunga Lipuli, Bandali amesema.

Mbao wapo vizuri.

Bandali amesema wataendelea kuiheshimu Mbao na kuiogopa, jambo ambalo linawafanya kucheza kwa tahadhali kubwa ili kupunguza makosa ambayo yanaweza kuwagharimu na kufungwa.

-Ni mchezo mgumu hasa, Mbao ni timu nzuri imekuja Mtwara ikihitaji kupata matokeo, lakini sisi tupo katika ardhi yetu ya nyumbani, tutapigana kwa mbinu zozote kuhakikisha tunapata matokeo, ameongeza.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Ndanda waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hata hivyo katika michezo sita ambayo Ndanda wamecheza kwenye uwanja wao wamefanikiwa kuibuka na ushindi mara moja pekee.

Mechi nyingine Jumamosi hii.

Lipuli FC Vs Mtibwa Sugar.

Stand United Vs Ruvu Shooting.

Related news
related/article
International News
Wolves sign Portugal international
8 hours ago
International News
Tough start for Gerrard as Rangers manager
15 Jun 2018, 12:10
FIFA World Cup
BREAKING: England ace set for a scan
1 hour ago
FIFA World Cup
Preview: Poland vs. Senegal - Prediction, team news and lineups
2 hours ago
FIFA World Cup
Cantona mocks Neymar haircut
4 hours ago