VPL: Mtibwa waihofia Lipuli

VPL: Mtibwa waihofia Lipuli

12 Jan 2018, 17:02

Kikosi cha Mtibwa Sugar tayari kipo mjini Iringa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara raundi ya 13 mzunguko wa kwanza dhidi ya wenyeji Lipuli FC mchezo utakaofanyika Jumamosi Januari 13.

Afisa Habari wa klabu ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligalambwike amesema wote waliosafiri wapo katika afya nzuri tayari kabisa kwa mchezo huo muhimu kwao utakaofanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa.

Amesema wanatambua umuhimu wa mchezo huo hasa baada ya Lipuli kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya wajelajela Tanzania Prisons, hivyo wamejiandaa vilivyo kuwakabili aliowaita faru waliojeruhiwa.

-Mchezo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na matokeo mabaya ambayo wenzetu wanapaluhengo waliyapata katika mchezo wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons, hivyo tunaamini wanaelekeza nguvu dhidi yetu, Kifaru amesema.

Waliosafiri

Kuelekea mchezo huo Shaban Hassan Kado amejumuishwa kwa mara ya kwanza katika safari za michezo ya ushindani ya Mtibwa Sugar tangu alipoumia katika mchezo wa kirafiki dhidi  ya Simba na pia Henry Joseph Shindika amejumuishwa

Kikosi cha Mtibwa kilichosafiri kuelekea Iringa kwa ajili ya mchezo huo ni makipa Shaban Hassan Kado na Benedictor Tinocco, Kwa upande wa mabeki ni Rodgers Gabriel , Hassan Mganga “Timbe”,  Dickson Job, Dickson Daud, Hassan Isihaka, Cassian Ponera “PEPE” na Hussein Idd Hante.

Viungo ni Shaban Mussa Nditi, Ally Makarani, Ismail Idan “Chomeka”, Saleh Khamis Abdallah, Hassan Dilunga, Mohamed Issa “MO Banka” na Henry Joseph Shindika, huku Washambuliaji ni pamoja na Hussein Javu, Riphat Khamis Msuya, Salum Kihimbwa na Haruna Chanongo.

Mtibwa Sugar hadi sasa imekusanya pointi 21 baada ya michezo 12 ya ligi kuu bara huku Lipuli ikikusanya pointi 14 baada ya michezo 12 ya ligi kuu bara ,Mtibwa Sugar inashikilia nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu bara na Lipuli wao wako katika nafasi ya 8.

Mechi nyingine Jumamosi hii.

Ndanda FC Vs Mbao FC.

Stand United Vs Ruvu Shooting

Related news
related/article
Local News
Wadada: I could not turn down Azam's offer
17 Jun 2018, 12:40
Local News
Onduparaka beat KCCA in Charity match
17 Jun 2018, 11:15
Transfer News
Brazil teenager chose Real Madrid over Barcelona
1 hour ago
FIFA World Cup
Preview: Russia vs. Egypt - Prediction, team news and lineups
4 hours ago
Local News
Kakamega Homeboyz coach blames late arrival for horrible defeat
2 hours ago