Mapinduzi Cup: Azam waiduwaza United na kutinga fainali

Mapinduzi Cup: Azam waiduwaza United na kutinga fainali

10 Jan 2018, 22:45

Timu ya soka ya Azam FC imeungana na URA ya Uganda kutinga kucheza hatua ya fainali ya michuano ya mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.

Azam imefanikiwa kuichapa Singida United kwa bao 1-0 katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliomalizika punde katika uwanja wa Amaan.

Licha ya Singida United kuonekana kumiliki mpira kwa asilimia kubwa lakini Azam waliibuka na ushindi kupitia bao pekee la Shabani Idd Chilunda katika dakika ya 79 ya mchezo kufuatia Makosa ya mlinzi Michael Lusheshangonga.

Aidha katika mchezo bao ulikuwa mkali na upinzani kwa timu zote mbili, mchezaji Shafik Batambuze aliyejiunga na Singida United akitokea Tusker FC ya Kenya alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo, hii ikiwa ni mara yake ya tatu kuchaguliwa katika mashindano hayo.

URA Vs Azam. 

Sasa Azam FC watacheza na URA katika mchezo wa fainali utakaopigwa Jumamosi ya Januari 13 mwaka huu katika uwanja wa Amaan kuanzia majira ya saa mbili na robo usiku.

Ikumbukwe URA wameingia hatua hiyo baada ya kuwatoa Dar Young Africans kwa penati 5-4 baada ya dakika za kawaida kumalizika kwa sare ya 0-0, katika mchezo ulioanza mapema jioni.

Related news
related/article
FIFA World Cup
Evra defends Pogba
17 Jun 2018, 18:40
FIFA World Cup
Group C Preview - Another French Revolution
12 Jun 2018, 08:15
FIFA World Cup
Cantona mocks Neymar haircut
4 hours ago
FIFA World Cup
Week 1 recap: Mexico shock Germany, as Portugal tie Spain
2 hours ago
FIFA World Cup
Messi responds to penalty miss
17 Jun 2018, 16:30