Mapinduzi Cup: Ni Yanga Vs URA, Singida Vs Azam nusu fainali

Mapinduzi Cup: Ni Yanga Vs URA, Singida Vs Azam nusu fainali

08 Jan 2018, 22:39

Singida United imefanikiwa kumaliza kileleni mwa kundi B katika michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.

Singida United wametoka sare ya 1-1 na Dar Young Africans katika mchezo wa mwisho wa kundi B uliomalizika punde katika uwanja wa Amaan Visiwani humo.

Singida United ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 72 kupitia kwa Daniel Lyanga Kwa kichwa safi kilichomshinda Mlinda mlango wa Yanga Rostand Youthe. Yanga walisubiri hadi dakika ya 90 kusawazisha bao hilo kupitia kwa Said Juma Makapu baada ya kuonganisha mpira wa faulo uliopigwa na Ibrahim Ajib.

Timu zote mbili zinafikisha Alama 13 lakini Singida United wanakaa kileleni kwa kuwa wanamtaji mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Mechi za nusu fainali. 

Nusu fainali ya kwanza itawakutanisha Yanga na URA wakati nusu fainali ya pili itawakutanisha Singida United na Azam na mechi zote zitafanyika Jumatano.

Fainali ya michuano hiyo itafanyika Januari 13 pamoja na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.

Related news
related/article
FIFA World Cup
The plight of goalkeepers at the World Cup
34 minutes ago
FIFA World Cup
Group E Preview : Unstoppable Brazil
12 Jun 2018, 12:30
Transfer News
Manchester United set record breaking price for Martial
2 hours ago
International News
Lemar signs Atletico deal, duo renews deals
8 hours ago
International News
Hazard addresses Real Madrid interest
22 hours ago