Majeruhi yamweka Nje Enock Atta Agyei dhidi ya Onduparaka FC.

Majeruhi yamweka Nje Enock Atta Agyei dhidi ya Onduparaka FC.

12 Aug 2017, 21:30

Mshambuliaji Kinda wa Wanarambaramba Azam FC, kutoka Nchini Ghana Enock Atta Agyei anaweza kuukosa mchezo wa Mwisho wa Kirafiki dhidi ya Ondurapaka kutokana na kuumia kifundo cha mguu katika mchezo wa jana dhidi ya URA.

Agyei alitoka katika dakika za mwisho katika mchezo walioshinda mabao 2-0, kutokana na majeraha hayo na hivyo kuna dalili kubwa kuukosa mchezo huo wa mwisho wa kirafiki ili kuhitimisha ziara yao nchini Uganda.

Meneja wa Azam FC Philipo Alando, ameuthibitishia Mtandao huu kwa Njia ya simu akiwa Kampala Uganda kuwa Agyei hatokuwepo katika benchi la Ufundi lakini kutokana na michezo waliyocheza mpaka sasa, Kocha Aristica Cioaba hatokuwa na kazi sana katika Kupanga kikosi.

-Wachezaji wote wanaendelea vizuri isopokuwa Agyei aliyeumia jana kwenye mchezo wetu dhidi ya URA, hivyo mechi ya kesho haitamuhusu, lakini lakuwaambia mashabiki wa Azam kuwa Timu kwa sasa inaonesha taswira njema, mwalimu ameshaanza kupata kikosi, ameshaona nani na nani wanaweza kucheza pamoja” Alando Amesema.

Msiwe na wasiwasi.

Katika hatua Nyingine Alando amewatoa hofu mashabiki wa Klabu hiyo kuwa wasiwe na wasiwasi katika msimu unaokuja kwani wanawachezaji wengi vijana ambao wanajuhudi kubwa hivyo watarajie matokeo mazuri.

-Katika wachezaji wote ambao tumewasajili hakuna mchezaji aliyezidi umri wa miaka 24, na kambi yetu huku umekwenda vizuri kabisa, tunapata mechi nzuri na majaribio sasa yote haya yamesaidia kuijenga timu yetu, tunawashukuru wamiliki wa timu kwa kukubali program hii, tunawaahidi kupambana” Alisema.

Wakiwa nchini Uganda, Azam FC imecheza michezo Mitatu hadi hivi sasa, ukiwemo mchezo dhidi ya Timu ya Taifa waliotoka sare ya 2-2, wakacheza na KCCA na kutoka sare ya 1-1 kabla ya jana kucheza na URA na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Related news
related/article
Transfer News
Chelsea confident of keeping Hazard
8 hours ago
FIFA World Cup
Mandzukic: Reaching World Cup final a 'miracle'
12 Jul 2018, 07:10
Transfer News
Ronaldo completes Juve medical
6 hours ago
FIFA World Cup
France defender retires from international football
15 hours ago
FIFA World Cup
French media on a high after France win
7 hours ago