CAF CL Yanga waifuata Rollers na matumaini kibao

CAF CL Yanga waifuata Rollers na matumaini kibao

13 Mar 2018, 06:07
Kikosi cha wachezi 20 pamoja viongozi 11 wa klabu ya soka ya Dar Young Africans wameondoka usiku huu kuelekea Mjini Gaborone, Botswana kucheza mchezo wa duru ya pili ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.

Mchezaji nyota na kinda wa Yanga Yussu Mhilu amesema wanaelekea Botswana wakiwa na matumaini makubwa ya kuweza kuibuka na ushindi ili kutinga katika hatua ya makundi ya ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu Afrika.

Mhilu amesema imani hiyo imetokana na kiwango kizuri walichokionesha katika michezo miwili ya ligi waliyocheza baada ya kufungwa na Rollers na kufanikiwa kushinda yote.

"Unajua mpira ni mchezo wa kupata morali, kushinda mechi hizi mbili mfululizo kumetujiengea kujiamini, wenzetu walifanikiwa kutumia nafasi hapa nyumbani, na sisi tunaimani kuwa hata kwao tunaweza kupata na kutumia nafasi na kupata ushindi," Mhilu amesema.

Ili kusonga mbele

Yanga wanahitaji ushindi wa mabao 2-0 au zaidi ili kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika au laa watatupwa nje na kuangukia katika michuano ya Shirikisho Afrika.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam Yanga walikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Township Rollers huku wakionesha mchezo dhaifu mbele ya watswana hao ambao walikuwa bora muda wote wa mchezo.

Wachezaji waliosafiri na timu

Msafara wa Yanga umeondoka usiku wa kuamkia Jumanne kupitia Addis Ababa nchini Ethiopia kabla ya kuonganisha ndege ya moja kwa moja hadi mjini Gaborone nchini Botswama.

Wachezaji ambao wameondoka ni pamoja na makipa, Ramadhani Kabwili na Youthe Rostand, wakati mabeki ni Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Gadiel Michael, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Patto Ngonyani na Kelvin Yondani.

Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Thaban Kamusoko, Pius Buswita, Raphael Daud, Yussuf Mhilu, Ibrahim Ajib, Said Mussa, Emmanuel Martin, Pappy Kabamba Tshishimbi, Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi.
Related news
related/article
FIFA World Cup
Ronaldo matches Pele, Puskas' records
16 Jun 2018, 09:05
International News
Egyptian giants, Al Ahly appoint Drogba's coach
12 Jun 2018, 19:55
Transfer News
Transfer Talk: Barca identifies Iniesta replacement, United hits brick wall in defender's pursuit
17 Jun 2018, 12:20
FIFA World Cup
Gareth Southgate hails England show
10 hours ago
FIFA World Cup
Preview: Belgium vs. Panama - Prediction, team news and lineups
19 hours ago