VPL: Yanga waitandika Stand United, kuwafikia Simba kileleni

VPL: Yanga waitandika Stand United, kuwafikia Simba kileleni

12 Mar 2018, 18:21

Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu soka Tanzania Bara Dar Young Africans wameitandika Stand United kwa mabao 3-1 katika mchezo raundi ya 22 uliopigwa jijini Dar es Salaam.

Yanga walikuwa wakihitaji ushindi katika mchezo huo ili kufungana pointi na wapinzani wao wakubwa Simba, licha ya kuwa mbele kwa mchezo mmoja.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Ibrahim Ajib, pamoja na Obrey Chirwa pamoja na lile la kujifunga la mlinzi wa Stand United Ally Ally.

Bao pekee la Stand United limefungwa na Vitalis Mayanga baada ya kipindi kirefu cha kulishambulia lango la Yanga ambalo lilikuwa imara na uhodari wa kipa Youthe Rostand.

Ushindi huo unawafanya Yanga kufikisha alama 46 na kuendelea kukalia katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Vikosi vilivyocheza:

Yanga SC: Youthe Rostand, Juma Abul Jaffary, Gadiel Michael Mbaga, Said Juma Makapu, Kelvin Yondani (C), Makka Edward, Yussuf Mhilu, Pius Buswita, Obrey Chirwa, Raphael Daud na Ibrahim Ajib Migomba.

Akiba: Ramadhank Kabwili, Hassan Ramadhan Hamis 'Kessy', Mwinyi Haji Mngwali, Nadir Haroub 'Cannavaro', Abdallah Shaibu, Thabani Kamusoko na Emmanuel Martin.

Stand United: Mohamed Makaka, Aaron Lulambo, Miraji Makka, Ally Ally, Erick Mulilo, Jisendi Maganga, Bigirimana Babikakule, Abdul Kasim, Ndikumana Raundi, Tariq Seif na Vitalis Mayanga.

Akiba: Frank Muwonge, Sixtus Sabilo, Ismail Gambo, Abdallah Juma, Ally Hamis na Makenzi Juma.

Mechi ya Jumanne, Machi 13.

Kagera Sugar Vs Mwadui FC (Kaitaba-Kagera)

Related news
related/article
Local News
Bidco United rope in six new players
19 minutes ago
FIFA World Cup
Another VAR intervention hands Sweden win over South Korea
16 hours ago
International News
Lemar signs Atletico deal, duo renews deals
3 hours ago
Transfer News
Transfer Talk: Barca identifies Iniesta replacement, United hits brick wall in defender's pursuit
17 Jun 2018, 12:20
FIFA World Cup
World Cup over for Croatia striker
14 hours ago