Kufanya vibaya kwa Kagera Sugar, Mexime amtupia lawama Mbaraka Yusuph

Kufanya vibaya kwa Kagera Sugar, Mexime amtupia lawama Mbaraka Yusuph

10 Mar 2018, 07:07

Kocha wa timu ya soka ya Kagera Sugar ‘Wanankurukumbi’ Mecky Mexime ameonesha kuMiss mshambuliaji Mbaraka Yusuph kutokana na kipaji chake cha kufumania nyavu anapokuwa uwanjani.

Mexime akizungumza baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Dar Young Africans amesema kama angekuwepo Mbaraka basi anaamini kabisa nafasi ambazo walizipata katika mchezo huo uliofanyika Ijumaa Machi 9 kwenye uwanja wa Taifa zingekuwa mabao.

“Mwaka jana tulikuwa na Mbaraka, ambaye mtu goli analijua, lakini mwaka huu tunakuja Mbaraka hayupo yani mtu ambaye ushamtengeneza unategemea akupe kitu hayupo, anakuja mwingine, inabidi umtengeneze upya sasa inategemea,” Mexime amesema.

Yanga wanawachezaji wazuri

Kocha huyo mzoefu wa soka la Tanzania amekisifu kikosi na wachezaji wa Yanga akiwaita wenye kuijua kazi yao, ambao wamekuwa hawana utani pale wanapokutana na goli, akilitaja hilo ndilo lililopelekea kupoteza mchezo huo licha ya kucheza vizuri.

“Wenzetu hizi timu kubwa wanawatu ambao wanaamua matokeo, hata muda wote hayupo kwenye mchezo lakini akipata nafasi hata moja tu, hiyo hiyo anaitumia, sisi tumecheza mpira lakini matokeo tumekosa,”amesema.

Msimu uliopita

Mbaraka alifunga mabao 12 katika msimu uliopita wa ligi akiichezea Kagera Sugar kabla ya kuondoka mwanzoni mwa msimu huu na kujiunga na mabingwa mara moja wa Tanzania Bara, Azam FC ya jijini Dar es Salaam.

Mbaraka aliiongoza Kagera Sugar kumaliza katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 53 lakini mpaka sasa msimu huu, Kagera Sugar wapo katika nafasi ya 14 na alama zao 18 huku wakiwa wamebakiwa na michezo 9 kabla ya kumaliza msimu.

Related news
related/article
International News
Arsenal duo resumes training
17 hours ago
International News
Mourinho surprised by Pogba's comments
14 Aug 2018, 15:35
Transfer News
Former Real Madrid coach linked with Man Utd
15 Aug 2018, 09:25
Transfer News
Arsenal legend reason for Fred snubbing Man City
15 Aug 2018, 19:45
International News
Former Arsenal striker close to Italian return
15 Aug 2018, 19:00