VPL: Yanga waipumilia Simba kisogoni, waitandika Kagera Sugar

VPL: Yanga waipumilia Simba kisogoni, waitandika Kagera Sugar

09 Mar 2018, 18:00

Ligi kuu soka Tanzania raundi ya 21 mzunguko wa pili  imeendelea kwa kasi kwa Mabingwa watetezi Dar Young Africans kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 3-0 dhidi ya wanankurukumbi Kagera Sugar.

Mchezo huo ambao umefanyika katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam umemaanisha kwamba Yanga wamezidi kuisogelea Simba kileleni, kwani kwa sasa tofauti ya alama baina yao zimebaki tatu kutoka saba za hapo awali.

Mchezo huo ambao ulikuwa mkali kwa kila upande kulishambulia lango la mwenzake, na kushuhudia kosa kosa za hapa na pale huku kipa wa Kagera Sugar Ramadhan Chalamanda akiokoa michomo hatari ya wachezaji Emmanuel Martin na Ibrahim Ajib.

Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko hakukuwa na timu yoyote ambayo ilifanikiwa kupata bao, huku Yanga wakionekana kuwa na asilimia kubwa za umilikaji wa mpira zaidi ya wageni Kagera Sugar.

Mabao ya Yanga

Yanga walipata bao la kwanza katika dakika ya 51 baada ya mwamuzi Shomari Lawi kuamuru penati baada ya mlinzi wa Kagera Sugar Mohamed Fakhi kunawa mpira ndani ya 18 akiwa katika juhudi za kuokoa shuti la Emmanuel Martin.

Penati hiyo ilikwenda kuchongwa na Ibrahim Ajib Migomba ambaye alipiga upande wa kulia wa mlinda mlango Ramadhan Chalamanda na kuandika bao la kuongoza kwa mabingwa hao watetezi.

Bao la pili katika mchezo huo lilifungwa katika dakika ya 77 baada ya walinzi kujisahau na kuruhusu krosi ya Ibrahim Ajib kumfikia Obrey Chirwa ambaye bila kutuliza alipiga V-Pass iliyomkuta Emmanuel Martin na kuukwamisha mpira nyavuni.

Yanga walipata bao la tatu baada ya kazi nzuri ya Yusuf Mhilu ambaye alipanda na mpira kwa kasi na kutoa pasi ambayo katika juhudi za kuuokoa mlinzi wa Kagera Sugar Juma Shemvuni alijikuta akimpoteza maboya kipa wake na mpira huo ukajaa kimiani.

Matokeo hayo yanawafanya Yanga kufikisha alama 43 na kukalia nafasi ya pili nyuma ya alama tatu dhidi ya Simba ambao wao wana alama 46 wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, wakati ambapo timu zote zimekwishakucheza mechi 20.

Vikosi vilivyocheza

Yanga SC: Youthe Rostand, Hassan Ramadhan Kessy, Haji Mwinyi, Said Juma Makapu, Kelvin Yondani, Patto Ngonyani/Makka Edward, Emmanuel Martin/Yusuph Mahadhi, Thaban Kamusoko/ Yusuph Mhili, Pius Buswita, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib.

Akiba: Ramadhan Kabwili, Juma Abdul, Gadiel Michael Mbaga, Nadir Haroub, Makka Edward, Juma Mahadhi na Yusuf Mhilu.

Kagera Sugar: Ramadhan Chalamanda, Mwaia Gereza, Adeyun Ahmed/Geofrey Taita, Juma Shemvuni, Mohamed Fakhi, Georeg Kavira, Japhet Makalai/Peter Mwalyanzi, Ally Nassor, Atupele Green/Omary Daga, Ally Makarani na Japhary Kibaya.

Akiba: Juma K Juma, Geofrey Taita, Abdallah Salumu, Uzoka Ugochukwu, Peter Mwalyanzi, Omary Daga na Paulo Ngalyoma.

Mechi za raundi ya 22, Jumapili Machi 11, 2018

AzamFC  vs Mbao FC (Azam Complex,Chamazi)

Ruvu Shooting vs Mbeya City  (Mabatini)

Singida United vs Ndanda  (Namfua)

Majimaji vs Lipuli  (Majimaji)

Tanzania Prisons vs Mtibwa Sugar (Sokoine)

Machi 13: Kagera Sugar vs Mwadui FC (Kaitaba)

Related news
related/article
International News
Best Bet Preview: Chelsea vs Arsenal
19 hours ago
International News
Celtic and Fenerbahce knocked out of Champions League
15 Aug 2018, 10:30
International News
Arsenal hit by major injury blow ahead of Chelsea clash
19 hours ago
International News
Sarri bans two Conte rules at Chelsea
15 Aug 2018, 12:50
International News
Former Arsenal striker close to Italian return
15 Aug 2018, 19:00