VPL: Mechi ya Simba na Njombe Mji yapigwa kalenda

VPL: Mechi ya Simba na Njombe Mji yapigwa kalenda

09 Mar 2018, 15:42

Mzunguko wa 22 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unatarajiwa kuendelea mwishoni mwa juma hili kwa michezo mitano ambapo mechi mbili za mzunguko huo zilizokuwa zichezwe Machi 11, 2018 zimebadilishiwa tarehe.

Simba waliokuwa wacheze ugenini dhidi ya Njombe Mji mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine baada ya Simba kuomba kusogezwa kwa mchezo huo ili kupata muda wa maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry utakaochezwa Port Said nchini Misri Machi 17, 2018.

Mchezo wa Kagera Sugar na Mwadui uliokuwa uchezwe Machi 11, 2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba sasa utachezwa Jumanne Machi 13, 2018 kutokana na kusogezwa kwa mchezo wao dhidi ya Dar Young Africans unaochezwa Ijumaa Machi 9, 2018.

Mechi zote tano

Mechi nyingine za mzunguko wa 22 zitakuwa kati ya Azam FC ambao watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex uliopo jijini Dar es Salaam kucheza na Wabishi Mbao FC.

Washika mitutu Ruvu Shooting ambao mchezo uliopita wametoka sare ya bao 1-1 na Singida United watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani kucheza na Mbeya City.

Mechi nyingine ni pamoja na Singida United ambao watacheza na Wanakuchele Ndanda FC katika uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Majimaji watawakaribisha Lipuli Fc katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Mechi nyingine ambayo itapigwa siku hiyo ya Jumapili ni ile ya Wajelajela Tanzania Prisons ambao watakuwa katika dimba la Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya Kucheza na Mtibwa Sugar.

Msimamo ulivyo

Mpaka sasa Simba ndio wanaoongoza kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 46 huku wakiwa wameshacheza michezo 20 wakati Azam wanafuatia wakiwa na alama 41 baada ya michezo 20 huku Yanga wakiwa nafasi ya tatu na alama zao 40.

Mkiani wapo Kagera Sugar ambao wanaalama 18 katika nafasi ya 14, wakifuatiwa na Njombe Mji ambao wana alama 18 katika nafasi ya 15 huku Majimaji wao wakishika mkia na alama zao 15.

Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Mabingwa Afrika wakati msimu huu ni timu mbili pekee ambazo ndizo zitakazoshuka daraja kupisha timu nne ambazo zitapanda daraja.

Related news
related/article
Transfer News
West Ham confident of signing Arsenal midfielder
17 hours ago
FIFA World Cup
Group H: The Group of talent
12 Jun 2018, 14:30
FIFA World Cup
Lukaku grabs brace as Belgium thrash resilient Panama
13 hours ago
FIFA World Cup
The curse of defending champions
21 hours ago
Transfer News
West Ham confident of signing Arsenal midfielder
17 hours ago