TPLB yapangua tena ratiba

TPLB yapangua tena ratiba

27 Feb 2018, 19:38

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya timu ya soka ya Simba SC na Stand United ya Shinyanga uliopangwa kufanyika Machi 4, mwaka huu umerudishwa nyuma kwa siku mbili hivyo utachezwa Ijumaa wiki hii (Machi 2, 2018).

Bodi ya Ligi imeamua kuurudisha nyuma mchezo huo wa nyumbani wa Simba, ili kuwapa fursa pana ya kujiandaa na mchezo wao wa Raundi ya kwanza kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya El Masry ya Misri.

Mabadiliko hayo yamegusa pia mechi kati ya timu ya soka Lipuli dhidi ya Ndanda FC ambayo nayo imesogezwa mbele hadi Machi 4, badala ya Mach 2 ya awali.

Mechi nyingine ni Kagera Sugar dhidi ya Mwadui FC ambayo ilipangwa kufanyika Mach 11, sasa imepelekwa mbele hadi Machi 13 na baada ya hapo, Ligi Kuu itakwenda mapumzikoni tena hadi Machi 22, ili kupisha mechi za kirafiki za kimataifa zilizo katika kalenda ya FIFA.

Yanga v Kagera Sugar

“Lakini Vilevile kulikuwa kuna mechi ambayo hatujaipa tarehe, na tumeipangia kwa sasa ni mechi ya raundi ya 21 kati ya Yanga na Kagera Sugar ambayo itachezwa tarehe tisa ya mwezi wa tatu,” Amesema mkurugenzi wa bodi ya ligi Boniface Wambura.

Ikumbukwe, Bodi ya Ligi pia imeahirisha mchezo mwingine wa Ligi Kuu kati ya  Mtibwa Sugar na Yanga SC ya Dar es Salaam uliopangwa kufanyika Machi 3, mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro umeahirishwa.

Nyuma ya pazia

Sababu za kuuahirisha mchezo huo namba 170 ni kuipa Yanga nafasi nzuri ya maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana Machi 6 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wakati Yanga wataikaribishaTownship Rollers ya Botswana Jumanne ya wiki ijayo, Simba SC watakuwa weneyji wa El Masry Jumatano wikiijayo, mechi zote zikichzwa wa Raifa, D res Salaam.

Related news
related/article
Local News
CECAFA Club: Ugandan giants eyeing glory in Tanzania
28 minutes ago
English Premier League
EPL 2018/19: Chelsea's Full Fixtures
14 Jun 2018, 12:55
International News
Wolves sign Portugal international
2 hours ago
International News
Arsene Wenger praises Kante
20 hours ago
FIFA World Cup
What went wrong for Brazil?
21 hours ago