Ndunguru: Yanga wameonja joto ya jiwe

Ndunguru: Yanga wameonja joto ya jiwe

26 Feb 2018, 09:25

Afisa Habari wa klabu ya soka ya Majimaji Onesmo Ndunguru amewabeza wale wote ambao walikuwa wakiwananga kwa kuwasimamisha wachezaji wao saba wa kikosi cha kwanza kuwa watakuwa mdembwedo kwenye mechi ya kombe la Shirikisho dhidi ya Dar Young Africans.

Ndunguru amesema wabaya wao wamepata aibu kubwa kwa namna ambavyo vijana wadogo wa Majimaji walivyoonesha kandanda la kuvutia ambalo almanusura liwaangamize Yanga.

"Tumewaprove watu wrong hasa wale ambao walikuwa wakitubeza katika mitandao ya kijamii na wamekutana na kikosi kikiwa ni tofauti kubwa, wengi walidhani tungetumia wachezaji wa kikosi B, ni kweli tumetumia baadhi yao," amesema.

Ndunguru ambaye timu yake imechapwa kwa mabao 2-1 amesema hayo ni sehemu ya matokeo, ambayo kiuhalisia yamekuwa tofauti kabisa na kile ambacho watu waliwatabiria kuwa watafungwa zaidi ya mabao matatu na kuendelea.

Tungefungwa nyingi! 

"Tumepoteza, tunashukuru tulichokipata, ukitazama katika mchezo huu hata kwenye safu yetu ya ulinzi watu wamezoea kuwaona Mahona na Kennedy Kipepe ambao hawapo na badala yao wamecheza Juma Salamba na Idrisa Mohamed ambao hawakuwahi kabisa kucheza pamoja na wamecheza vizuri hilo tunashukuru sana, kwa matarajio yalikuwa Yanga wangepata mabao mengi" ameeleza.

Dhidi ya Kagera Sugar 

Katika hatua nyingine Ndunguru amesema matokeo hayo wanayasahau na sasa wanaelekeza nguvu zao katika mchezo ujao wa ligi dhidi Kagera Sugar utakaofanyika mjini Bukoba.

Ndunguru amedadavua kuwa wanajua wapo katika nafasi mbaya sawa na wapinzani wao na ushindi ndio njia pekee ambayo itawaondoa huko mkiani, hivyo watasafiri mapema na kuanza maandalizi mapema ya mchezo huo.

Majimaji wapo katika nafasi ya 15 wakiwa na alama 15 baada ya michezo 19, Huku wapinzani wao Kagera Sugar nao wakiwa katika nafasi ya 14 na alama zao 15 pia.

Related news
related/article
International News
Guardiola lauds Sterling after Arsenal win
13 Aug 2018, 08:05
International News
Mourinho reveals players to miss Leicester clash at Old Trafford
10 Aug 2018, 11:00
International News
Casemiro: Real Madrid has moved on from Ronaldo
21 hours ago
International News
Who has the best MEGA JACKPOT offer?
20 hours ago
International News
BREAKING: Kevin De Bruyne suffers knee injury
15 Aug 2018, 18:10