VPL: Yanga waikung'uta Majimaji, kujiimarisha katika nafasi ya tatu

VPL: Yanga waikung'uta Majimaji, kujiimarisha katika nafasi ya tatu

14 Feb, 17:54

Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu soka Tanzania Bara, Dar Young Africans wameendelea kuchanja mbuga katika harakati za kutetea taji lao baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Wanalizombe Majimaji FC.

Katika mchezo huo Majimaji walionekana dhohofu ili hali kwa dakika nyingi za mchezo kwa kucheza takribani dakika 70 wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao Mpoki Mwakinyuke kupewa kadi nyekundu katika mchezo ambao umefanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam 

Yanga iliwachukua dakika 20 kuandika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi.

Penati hiyo ilipatikana baada ya mlinzi Mpoki Mwakinyuke kuunawa mpira ndani ya 18 akiwa katika harakati za kuuzuia mpira wa Obrey Chirwa.

Kwa tukio hilo mwamuzi Nassoro Mwinchui ilibidi amuoneshe Mwakinyuke kadi nyekundu kwa tukio hilo na kuwazawadia Yanga penati hiyo.

Dakika 9 baadae Yanga waliandika bao la Pili kupitia kwa Obrey Chirwa baada ya kupokea krosi ya Gadiel Michael na kupiga kichwa ambacho kilimshinda kipa Salehe Malande.

Yanga walipata Bao la tatu dakika moja kabla ya kwenda mapumziko kwa shuti la guu la kulia la Emmanuel Martin, nje ya 18 ambalo kabla ya kuzama wavuni mpira ulibusu kidogo mwamba.

Bao la Majimaji 

Majimaji walikianza kipindi cha pili kwa kasi na kulishambulia lango la Yanga, jambo ambalo liliwapa faida katika dakika ya 55 kwa kupata penati.

Penati hiyo ilipatikana baada ya mlinzi wa Yanga Juma Makapu kunawa ndani ya 18 katika harakati za kuuondoa mpira langoni mwake penati ambayo ilienda kuchongwa na Marcel Boniventure na kuwapatia Majimaji bao la kwanza.

Tshishimbi tena 

Siku hii ya wapendanao ilikuwa njema Sana kwa Pappy Kabamba Tshishimbi kwani katika dakika ya 84 alifanikiwa kufunga bao la pili kwake na la nne kwa Yanga baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 na kujaa moja kwa moja nyavuni.

Licha ya kupigwa mabao yote hayo Majimaji walijaribu kuisakama ngome ya ulinzi ya Yanga, na mara kadhaa wachezaji Jaffary Mohamed na Peter Mapunda kumjaribu kipa Ramadhan Kabwili.

Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga walitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-1 na kuwafanya kufikisha alama 37 wakiwa nyuma ya Simba kwa alama 4 wenye alama 41 ambao watakuwa na kibarua dhidi ya Mwadui siku ya Alhamis.

Vikosi vilivyocheza 

Yanga: Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Said Makapu, Andrew Vincent/ Nadir Haroub, Makka Edward, Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita/Juma Mahadhi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib/ Geofrey Mwashiuya na Emmanuel Martin.

Akiba : Benno Kakolanya, Juma Abdul,Haji Mwinyi, Raphael Daud, Geofrey Mwashiuya Nadir Haroub na Juma Mahadhi

Majimaji: Salehe Maland, Aziz Sibo, Mpoki Mwakinyuke, Kennedy Kipepe, Paulo Maona, Hassan Hamis, Peter Mapunda, Yakubu Kibiga/ Geofrey Mlawa, Six Mwasekaga/ Alex Kondo, Marcel Boniventure/ Lucas Kikoti na Jaffary Mohamed.

Akiba: Hasheem Musa, Sadick Gawaza, Alex Kondo, Lucas Kikoti, Geofrey Mlawa, Jerryson Tegete na Paul Lyungu.

Related news
related/article
Local News
Gor Mahia ready for Assad clash
26 May, 20:30
Local News
Matano:Tusker will be better in the second leg
26 May, 14:55
Local News
Mdluli happy with his team's defending against Harambee Stars
26 May, 13:30
International News
Germany coach prefers Messi to Ronaldo
26 May, 08:30
Local News
Gor Mahia ready for Assad clash
26 May, 20:30