Ally Bushiri kocha mpya Njombe Mji FC

Ally Bushiri kocha mpya Njombe Mji FC

11 Feb, 14:53

Timu ya Njombe Mji ya kutoka mkoani Njombe imemteua Ally Bushiri kuwa kocha mkuu wa timu hiyo ambapo anatarajiwa kuanza kazi mara moja. Akithibitisha taarifa hizo Mwenyekiti wa Njombe Mji Erasto Mpete, amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuinusuru timu hiyo kushuka daraja msimu ujao kufuatia matokeo mabovu wamekuwa wakiyapata. 

"Kwa kuongeza nguvu hii ya Ally Bushiri tunaamini kabisa timu yetu itafanya vizuri mashabiki wamekuwa wakitaka timu kupata matokeo lakini ni kitu hawajakuwa wakipata", amesema Mpete.

Kwa upande wake kocha Ally Bushiri ameahidi mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kutarajia mabadiliko ambayo yatasaidia kurejesha imani yao kwa Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza. 

"Naamini kwamba kwa ujio wangu tutaanza kuona mabadiliko ya ni aina fulani kitu cha msingi cha kufanya ni kuhakikisha unacheza mpira ndani ya kiwanja kwa ajili ya kupata matokeo ili kupelekea mafanikio ya nje ya kiwanja kwa sababu football without fans is not football", amesema Bushiri. 

Kocha hiyo zamani akiifundisha timu ya Mwadui amesema kibarua kigumu ni kubadilisha mfumo wa wachezaji hao na kuufanya wa kasi na wa kushambulia ili wapate matokeo. 

Mfumo

"Lazima tucheze attack football , very fast football tuns attack tunarudi kwa sababu saivi timu inacheza lakini inacheza short pass haiko fast tunataka tuongeze speed", ameahidi Bushiri. 

Njombe Mji ambao wanavuta mkia wa msimamo wa ligi Kuu soka Tanzania Bara wakiwa na alama 13 wanashuka dimbani Jumapili dhidi ya timu ya Mbeya City katika mchezo ambao utafanyika kwenye uwanja wa saa Sabasaba mkoani Njombe.

Related news
related/article
International News
Van Dijk reveals why he joined Liverpool
2 hours ago
International News
Mbappe rejected Real Madrid
6 hours ago
International News
Ronaldo compares Salah with Messi
25 May, 09:20
International News
New Arsenal boss Unai Emery's top five past signings
25 May, 09:00
International News
Fred to keep United waiting
25 May, 08:55