Bocco ndiye mchezaji bora wa ligi mwezi Januari

Bocco ndiye mchezaji bora wa ligi mwezi Januari

11 Feb, 10:14

Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya soka ya Simba John Raphael Bocco, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa kuwashinda wachezaji wawili walioteuliwa kuwania tuzo hilo.

Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kumshinda mwenzake Emmanuel Okwi wa Simba SC na Awesu Awesu wa Mwadui FC baada ya kuchaguliwa na kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.

Bocco amekuwa na msaada mkubwa kwa timu hiyo akiisaidia Simba SC kupata alama tisa katika michezo mitatu waliyopata ushindi akifunga mabao matatu pamoja na kutoa pasi mbili za usaidizi wa bao. 

Simba iliifunga Singida United mabao 4-0, ikaifunga Kagera Sugar mabao 2-0 na kisha ikailaza Majimaji mabao 4 - 0. 

Kwa kutwaa tuzo hiyo kama ilivyokawaida Bocco atazawadiwa fedha taslimu shilingi milioni moja kutoka kwa Mdhamini Mkuu wa Ligi, Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kisimbusi kutoka kwa wadhamini wengine Azam TV.

Wachezaji waliowahi kutwaa tuzo

Wachezaji wengine ambao tayari wametwaa tuzo ya mwezi kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi (Agosti), Shafiq Batambuze (Septemba), Obrey Chirwa (Oktoba), Mudathir Yahya( Novemba) na Habibu Haji Kiyombo (Disemba).

Related news
related/article
International News
Barcelona defender hails Griezmann
6 hours ago
International News
Fred to keep United waiting
25 May, 08:55
International News
Former Spain coach showers praise on Real Madrid
23 May, 09:00
International News
Muller: Salah a big candidate for Ballon d'Or
25 May, 08:20
International News
Bologna confirm Donadoni departure
24 May, 19:56