Nsagijwa: Yanga tumejiwekea mazingira magumu

Nsagijwa: Yanga tumejiwekea mazingira magumu

11 Feb, 10:20

Kocha msaidizi wa kikosi cha timu ya soka ya Dar Young Africans Shadrack Nsajigwa, amekiri kuwa wamejiweka katika mazingira magumu kwa kushindwa kuwafunga mabao mengi wapinzani wao katika Michuano ya klabu bingwa Barani Afrika, Saint Louis ya Shelisheli watakapokutana katika mchezo wa marudiano.

Nsajigwa ambaye timu yake iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1 - 0 lililofungwa na Juma Mahadhi katika dakika ya 67, amesema kuwa walipanga kucheza mchezo wa mashambulizi kwa lengo la kupata mabao mengi lakini wapinzani wao wakawasoma mapema na kuamua kucheza sana nyuma bila kufunguka na kufanya mchezo huo kuwa mgumu.

"Tulicheza kushambulia ili tupate magoli mengi lakini wapinzani wetu wakatumia mbinu ya kucheza nyuma ya mpira, wametupa ugumu na ndio maana tumepata ushindi mwembamba tuna mshukuru Mwenyezi Mungu na tuna imani watafunguka wakicheza nyumbani na sisi tutatumia nafasi hiyo", amesema Nsajigwa. 

Mechi ya marudiano

Timu hizo zitarudiana tena Februari 20 mjini Victoria nchini Shelisheli katika mchezo ambao Yanga watahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ili kujihakikishia kufuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo.

Related news
related/article
International News
WC 2018: Salah injury update
4 hours ago
International News
Ronaldo: I can't be compared with Salah
25 May, 14:25
International News
Arsenal new boss recalls forgotten forward
24 May, 10:45
International News
Man United and Real Madrid favourite Beckham begs Zidane to beat Liverpool
25 May, 17:36
International News
Reus relishing Favre reunion at Borussia Dortmund
25 May, 19:33