CAF CL: Yanga waidungua St Louis, Zesco wakibanwa na JKU

CAF CL: Yanga waidungua St Louis, Zesco wakibanwa na JKU

10 Feb, 17:50

Mabingwa wa Tanzania Bara Dar Young Africans wameanza vyema michuano ya ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuwachapa mabingwa wa Shelisheli St Louis katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ambao walihitaji ushindi mnono, wameshindwa kufanya hivyo baada ya kupata bao moja pekee licha ya kucheza soka safi ndani ya dakika zote 90.

Yanga walianza kufanya mipango ya kutafuta bao la mapema ili kuweza kuwachanganya wageni St. Louis kwani katika dakika ya pili tu Papy Kabamba Tshishimbi na Emmanuel Martin walipiga mashuti kuelekea langoni mwa wageni.

Dakika ya saba St Louis walifanya shambulizi nzuri lakini mabeki wa Yanga walisimama imara na kuondoa hatari hiyo.

Yanga ilikuwa kidogo tu waandike bao la kuongoza katika dakika ya 15 baada ya Pius Buswita kushindwa kuonganisha kwa kichwa mpira wa kona uliochongwa na Ibrahim Ajib.

Penati ya Chirwa 

Katika dakika ya 23 Hassan Kessy Ramadhan akiwa anajaribu kinatoka mabeki wa St Louis Herve Patorogang akamkwatua ndani ya 18 na mwamuzi akaamuru Kupigwa penati ambayo ilienda kuchongwa na Obrey Chirwa ambaye hakufanikiwa kufunga badala yake akautoa mpira nje.

Kukosa huko kunamfanya Obrey Chirwa kukosa penati yake ya tatu kwa kipindi cha hivi karibuni katika penati sita ambazo amezipiga mpaka sasa.

Yanga waliendelea kulishambulia lango la St Louis lakini mara katika dakika ya 30 shuti la Kelvin Yondani, Faulo ya Gadiel Michael, na nafasi ya wazi ya Ibrahim Ajib dakika ya 33 zilishindwa kuzaa bao lolote.

Kosakosa hizo langoni mwa St Louis ambao walipaki bus ziliendelea hadi dakika 45 zilipomalizika na timu kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili St Louis waliingia wakiwa tofauti kidogo kwa angalau dakika 10 za mwanzo walikuwa wakipiga pasi fupifupi na zilizokuwa na macho lakini walishindwa kuipita safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na Juma Makapu na Kelvin Yondani.

Makosa ya Kabwili 

Mashambulizi hayo yalizidi na pengine wangeandika bao la kuongoza katika dakika ya 54 baada ya mpira uliochongwa kumkuta Kipa Ramadhan Kabwili na yeye pasipo kuwa makini ukamtoka mikononi mwake na kumkuta kiungo wa St Louis ambaye naye alipiga shuti likatoka nje.

Kosakosa ya Ajib 

Yanga walikosa nafasi nzuri ya kupata bao Ibrahim Ajib akiwa yeye na kipa baada ya kupokea pasi mparazo kutoka kwa Obrey Chirwa anapiga kwa hasira na mpira unapaa kuu langoni mwa St Louis.

Hali hiyo ikiwafanya Yanga kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Ibrahim Ajib na Emmanuel Martin na kuwaingia Geofrey Mwashiuya na Juma Mahadhi.

Bao la Mahadhi 

Mabadiliko hayo yalisaidia Kwani haikupita hata sekunde 30, Yanga waliandika bao kupitia kwa Juma Mahadhi kufuatia mpira wa kona uliochongwa na Geofrey Mwashiuya ikiwa ni dakika ya 67.

Baada ya bao hilo timu zote zilianza kucheza kwa kasi ndogo licha ya mara moja moja Yanga kulishambulia lango la St Louis huku wageni wenyewe wakipanda langoni mwa Yanga kwa kushtukiza.

Lakini baadae Yanga wakafanya mabadiliko ya mwisho kwa kumtoa Pius Buswita na kumuingiza kinda Yusuf Mhilu ikiwa ni dakika ya 86.

Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga walitoka kifua mbele kwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kujiwekea mazingira magumu ya kufuzu hatua inayofuata.

Timu hizo zitarudiana tena Februari 20 mjini Victoria nchini Shelisheli katika mchezo ambao Yanga watahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ili kujihakikishia kufuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo.

JKU 0-0 Zesco United.

Wakati huo huo mabingwa wa soka Visiwani Zanzibar, JKU wamelazimishwa sare wakiwa nyumbani na Zesco United ya kutoka nchini Zambia katika mchezo ambao umefanyika kwenye uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Maafande hao wa kujenga uchumi Zanzibar, watakuwa na nafasi nzuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kama watafanikiwa kupata sare ya mabao au ushindi wa aina yoyote katika mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki moja baadae mjini Lusaka.

Iwapo JKU watafanikiwa kupitia hatua hiyo ya awali watakutana na BENIN ya Benin au Asec Mimosas ya Ivory Coast katika hatua ya kwanza.

Related news
related/article
International News
Ramos wishes Salah quick recovery
9 hours ago
International News
CL Final:Liverpool boss expects his side to be brave
26 May, 08:15
International News
Koscielny reveals his remedy to World Cup heartache
24 May, 16:40
International News
Salah's long-term potential 'not important', says focused Klopp
25 May, 18:28
International News
Gudjohnsen tips Madrid to beat Liverpool, despite star trio
26 May, 11:49