CAF CL: Pacha wake Chirwa arejea kuwavaa St Louis

CAF CL: Pacha wake Chirwa arejea kuwavaa St Louis

10 Feb, 13:31

Mshambuliaji Ibrahim Ajib wa Dar Young Africans amepangwa kuanza katika katika kikosi cha kwanza kinachoshuka dimbani jioni hii kuumana na Saint Louis ya Shelisheli katika hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa Barani Afrika.

Ajib sambasamba na Obrey Chirwa ndio watakaoongoza safu ya ushambuliaji wakati ambapo Nadir Haroub Canavaro amepangwa kuanzia benchi.

Licha ya taarifa ya klabu hapo Ijumaa kutaja kuwa Kipa Youthe Rostand amepata nafuu kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Lipuli, lakini hayupo kabisa katika kikosi cha leo na hivyo kinda Ramadhan Kabwili ameanza huku benchi akikaa Beno Kakolanya.

Kinachoanza: Ramadhani Kabwili, Hassan Ramadhan Kessy, Gadiel Michael Mbaga, Kelvin Patrick Yondani, Said Juma Makapu, Papy kabamba Tshishimbi, Pius Buswita, Raphael Daud Loth, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib Migomba na Emmanuel Martin.

Akiba: Beno Kakolanya, Juma Abdul, Nadir Haroub, Juma Mahadhi, Geoffrey Mwashiuya, Said Mussa na Yusuf Mhilu.

Mchezo huo mkali utafanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Related news
related/article
International News
Barcelona defender hails Griezmann
7 hours ago
International News
Ronaldo: I can't be compared with Salah
25 May, 14:25
International News
New Arsenal boss Unai Emery's top five past signings
25 May, 09:00
International News
Spalletti in 'no rush' to sign new Inter deal
24 May, 19:31
International News
FA condemns assault of match official
24 May, 20:18