Ratiba VPL, nyakati za furaha kurejea Kagera?

Ratiba VPL, nyakati za furaha kurejea Kagera?

10 Feb, 10:34

Raundi ya 18 mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea Jumapili ya Februari 11 kwa michezo minne kufanyika katika viwanja mbalimbali nchini.

Katika uwanja wa Namfua mjini Singida, Wapiga debe Stand United baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Lipuli watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Singida United.

Singida United wanauendea mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kuichapa Mbao kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopita.

Wanatamtam wao wamesafiri hadi jijini Mwanza kukipiga na wabishi Mbao FC mchezo ambao utafanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika uwanja huo Mbao FC waliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0, lakini sasa Mtibwa watakuwa na maswali mengi kuruhusu kufungwa na Mbao kwani wamepoteza michezo miwili mfulululizo mpaka sasa.

Wanakuchele Ndanda FC wao watakuwa uwanja wao wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara kucheza na wakongwe Tanzania Prisons.

Tanzania Prisons na Ndanda wanauendea mchezo huo wakiwa na matokeo sawa katika michezo iliyopita kwani kila timu ilitoka sare, Tanzania Prisons wakitoka sare ya 0-0 na Majimaji na Ndanda waliambulia sare ya 2-2 na Mbeya City.

Njombe Mji v Mbeya City 

Njombe Mji baada ya kupokea kisago kutoka kwa Yanga juma lililopita, wanarejea nyumbani katika uwanja wa Sabasaba kucheza na Wanakomakumwanya Mbeya City.

Njombe Mji ndio timu inayoshika mkia mkiwa na alama 13 hivyo ushindi katika mchezo huo ni muhimu ili kujiondoa mkinipa mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Wanapaluhengo Lipuli FC watacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.

Kila timu inachachu ya ushindi kwani katika michezo iliyopita walipata matokeo, Lipuli wakiichapa Stand United mabao 3-0 huku Ruvu Shooting wakiitandika Kagera Sugar mabao 2-0.

Kagera v Azam 

Jumatatu kutakuwa na mchezo mmoja ambapo Azam FC watakuwa Bukoba kwenye uwanja wa Kaitaba kuumana na Kagera Sugar ambao msimu huu wamekuwa jamvi la Kibarazani.

Azam baada ya kuchapwa na Simba wamesafiri Jumamosi hii kwenda Bukoba kusaka alama tatu ili kuweza kujihakikishia nafasi nyingine ya kutwaa taji la ligi.

Yanga v Majimaji 

Ligi hiyo itaendelea Jumatano ambapo mabingwa watetezi Dar Young Africans watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Taifa kucheza na Majimaji FC.

Raundi ya 18 itahitimishwa siku ya Alhamis Februari 15 kwa mchezo mkali ambapo Mwadui FC watacheza na Simba SC ambao Ndio vinara wa ligi katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.

Msimamo bado unaonesha Simba wanaongoza wakiwa na alama 41 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 34 wakati Azam na Singida United wakifuatiwa wakiwa na alama 33 kila mmoja.

Related news
related/article
International News
UEFA CL: Real Madrid v Liverpool the key battles
25 May, 17:00
International News
Football legend set to marry two women at same time
24 May, 14:40
International News
Ancelotti delighted with return
24 May, 08:55
International News
Ronaldo's rival Salah shifts focus back to Liverpool versus Real Madrid
25 May, 14:34
International News
Great players have to play here - Real Madrid's Marcelo continues Neymar courtship
25 May, 16:18