CAF CL: JKU, Zesco United warushiana maneno

CAF CL: JKU, Zesco United warushiana maneno

09 Feb, 19:31

Kocha mkuu wa timu ya soka ya jeshi la kujenga Uchumi Zanzibar ‘JKU’ Ali Suleiman Mtuli amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri na wanamatumaini makubwa yakufanya vyema katika mchezo wa hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia.

Mtuli amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wanategemea ushindi mzuri kwani wachezaji wote ni wazima na hata wale ambao walikuwa na majeraha tayari wamerejea kwenye kikosi.

Amesema atatumia mfumo wa jadi ndani ya klabu ya JKU wa 4-2-3-1 ambao utakuwa mfumi mzuri kuweza kuwakabili Zesco ambao amewataja kuwa ni timu nzuri na ambayo haifungiki kirahisi.

“Plan ya mchezo huo ni 4-2-3-1, ambayo imezoeleka katika timu yetu, na vile vile nimeipitia kwa kipindi kirefu kulingana na Zesco jinsi gani wanavyocheza, ninachosema ni kuwa nawaomba mashabiki waje kwa wingi na kuishangilia timu yao kwani naamini kabisa tunaenda kuibuka na ushindi katika mchezo huo,” Mtuli ameeleza.

Zesco wanasemaje?

Kwa upande wake kocha wa Zesco United Tenant Chembo, amesema mazingira ya Zanzibar yamekuwa rafiki kwao toka walipokuja na kitu ambacho kinazidi kuwapa moyo kuwa mchezo huo utakuwa mzuri na kuvutia.

Chembo amesema hawataidharau JKU kwa namna yoyote ile kwa kuwa ni mabingwa wa Zanzibar na kwamba wapo tayari kwa mpambano huo ili kuweza kushinda na kufikia malengo yao waliyojiwekea.

“Kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo, tunahitaji kuwapa heshima yao kwani hatuwajui, hatujui soka lao lipoje lakini ni muhimu tukawa na mkazo wa kile tulizokifuata huku, kwa timu lakini pia kwa kila mtu mmoja mmoja, hakika tumejiandaa,” Chembo alieleza.

Nafasi ya JKU

JKU watacheza na Zesco katika mchezao mkali ambao unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Amaan uliopo mjini Unguja ukiwa ni mchezo wa kwanza kabla ya wiki mbili baadae kurudiana huko nchini Zambia.

Ili kujihakikishia kufuzu katika hatua inayofuata, JKU watalazimika kushinda kwa idadi kubwa ya mabao na ikibidi kutoruhusu kufungwa bao lolote, jambo ambalo litawatengenezea mazingira ya kufuzu hatua ya kwanza.

JKU wakifanikiwa kupitia hatua hiyo ya awali watakutana na BENIN ya Benin au Asec Mimosas ya Ivory Coast katika hatua ya kwanza.

Related news
related/article
International News
UEFA CL: Real Madrid v Liverpool the key battles
22 hours ago
International News
Iniesta's Vissel Kobe move confirmed
24 May, 11:35
International News
Midfielder accuses referee of 'robbing' Roma
23 May, 11:25
International News
Buffon in consideration for Italy call, says Mancini
24 May, 16:10
International News
Istanbul to host 2020 Champions League final
24 May, 17:17