Leodgar Chilla Tenga, mwenyekiti mpya BMT

Leodgar Chilla Tenga, mwenyekiti mpya BMT

09 Feb, 16:39

Rais wa heshima wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini ‘TFF’ Leodigar Chilla Tenga ameteuliwa na waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa mwenyekiti mpya wa baraza la Michezo la Taifa ‘BMT’.

Waziri Mwakyembe ametumia nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria ya BMT ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ikisomwa na muundo wa shughuli za baraza kufanya uteuzi huo Februari 9, 2018.

Tenga ambaye aliwahi kuwa rais wa TFF kwa kipindi cha miaka nane kutoka mwaka 2005 hadi mwaka 2013 kwa kumpisha Jamal Malinzi.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu za Young Africans na Pan African FC, pamoja na Taifa Stars aliwahi pia kuwa mjumbe wa BMT kwa kipindi cha kati ya mwaka 1990 hadi 2002 kabla ya uteuzi huu wa kuwa mwenyekiti.

Wajumbe wengine

Tenga atakuwa pamoja na wajumbe wengine tisa ambao wameteuliwa na Waziri Mwakyembe kuunda baraza jipya la michezo nchini kufuatia kuvunjwa kwa lile la awali katikati ya mwa mwaka jana.

Wajumbe hao ni pamoja na Prof. Mkubwa Mtambo, Bi. Beatrice Singano, Kanali Mstaafu Juma Ikangaa, John Joseph Ndumbaro, Rehema Sefu Madenge na Salmin Kaniki,.

Kadhalika wajumbe wengine ni Yusuph Singo (Mkurugenzi wa Maendeleo ya michezo wa Wiazar), Dkt. Edicome Shirima (Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi) na Mohamed Kiganja ambaye ni katibu mkuu wa BMT.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ni kwamba uteuzi wa wajumbe wote umeanza rasmi Februari 8, 2018 na watalitumikia baraza kwa kipindi cha miaka mitatu.

Dioniz Malinzi

Ikumbukwe Julai mwaka jana Waziri wa Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alingaza kusitisha uteuzi wa Mwenyekiti, Dionis Malinzi pamoja wajumbe wote kwa sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kutatua migogoro ya michezo nchini.

Related news
related/article
Local News
Ramos wishes Salah quick recovery, dismisses ‘intentional’ foul play talks
4 hours ago
International News
Bale strikes twice as Madrid lifts 3rd straight UCL trophy
18 hours ago
International News
Iniesta's Vissel Kobe move confirmed
24 May, 11:35
Local News
Vipers are 2017-18 Uganda Premier League champions
25 May, 21:05
International News
People like to talk - Marcelo responds to misquoted Klopp
25 May, 20:35