CAF CL: Kumbe St Louis washaisoma Yanga, wanaijua A-Z

CAF CL: Kumbe St Louis washaisoma Yanga, wanaijua A-Z

09 Feb, 09:00

Mshauri wa ufundi wa klabu ya soka ya St Louis ya Ushelisheli Ulrie Mathios amewataja Yanga kuwa ni timu ngumu na watahitaji kujituma zaidi ili kuweza kupata ushindi.

Amesema tayari wameshaangalia mikanda ya video inayohusu mechi za Yanga na wameshawatambua Wacheza hatarishi kwao na wanalifanyia kazi suala la kuweza kuwakabili wasilete madhara.

"Siwezi kuwataja wachezaji ambao tumewatambua kwa kuwa hii kidogo ni siri ya benchi la ufundi, na tumewaona kupitia video zao hasa za mwaka jana, kiukweli ni timu nzuri," amesema. 

Ameongeza kuwa iliwabidi pia kuutazama mchezo wa Simba na Azam ili kufahamu soka la Tanzania na kidogo wameng'amua mambo ambayo yatawasaidia katika mchezo wao wa Jumamosi.

"Tumeuona kipindi cha kwanza cha mchezo wa Simba na Azam, kwa kile ambacho tumekiona kwenye mchezo ule kimetupa hali ya kujiamini kwa kuwa kidogo tumefahamu kuhusu soka la Tanzania," amesema.

Yanga wananafasi ya kushinda 

Kadhalika amesema kuwa Yanga watakuwa na nafasi kubwa ya kupata matokeo mazuri kwa kuwa walikuwa kwenye mechi za ushindani kwa muda mrefu tofauti na wao ambao wapo katika mapumziko ya ligi toka Disemba mwaka jana.

St Louis wapo nchini toka Jumanne wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume uliopo katika ofisi za Shirikisho la soka nchini 'TFF'.

Mchezo wa Dar Young Africans na St Louis utakuwa ni mchezo wa hatua ya awali ya michuano ya klabu Bingwa Afrika, mchezo ambao utafanyika Februari 10 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Related news
related/article
International News
Low: Neuer will not be a World Cup back-up
18 hours ago
International News
UEFA CL: Mane sends gifts back to the village
25 May, 15:05
International News
Arsenal new boss recalls forgotten forward
24 May, 10:45
International News
Salah's long-term potential 'not important', says focused Klopp
25 May, 18:28
International News
It's funny if two managers in the final have no clue about tactics - Klopp defends Zidane
25 May, 18:33