Kocha wa Mwadui aridhishwa na kiwango cha wachezaji

Kocha wa Mwadui aridhishwa na kiwango cha wachezaji

09 Feb, 09:20

Kocha mkuu wa Timu ya Mwadui Ally Bizimungu amefurahia mwenendo wa timu hiyo na kusema kuwa endapo wataendelea hivyo bila shaka watamaliza katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Bizimungu amesema japo wamekuwa wakicheza vizuri hawakuwa na uwezo wa kumalizia na kupoteza mabao mengi ambayo amesema yangewasaidia.

"Timu iko na improvement wachezaji wamekuwa waskivu na wanacheza kwa maelekezo siku zote tumekuwa tukicheza vizuri lakini tatizo imekuwa umaliziaji tunashindwa kufunga mabao hata tukipata nafasi za wazi lakini sasa ukiangalia tunafunga mabao", amesema Bizimungu. 

Kocha huyo raia wa Rwanda amewaomba mashabiki wa Mwadui Fc kuendelea kuwaunga mkono ata wakati wanateleza ili kuwapa wachezaji motisha ya kuendelea kufanya vizuri. 

"Siku zote mchezo una matokeo matatu kufunga, kufungwa na kugawa wapenzi na mashabiki wa Mwadui wasihofu chochote timu iko vizuri wachezaji wapo vizuri waendelee kutupa sapoti siku zote ata wakati tunashindwa nasi tutapambana tufanye vizuri", ameongeza Bizimungu. 

Mwadui Fc wanashika nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 18.

Michezo mitano ya Mwadui iliyopita

Mwadui 3 - 1 Mtibwa Sugar

Singida United 3 - 2 Mwadui

Mwadui 2 -2 Njombe Mji 

Mwadui 1 - Ndanda

Yanga 0 - 0 Mwadui

Related news
related/article
International News
Low: Neuer will not be a World Cup back-up
18 hours ago
International News
WC 2018: Germany coach defends Ozil,Gundogan
24 May, 15:40
International News
UEFA CL: How Soton will benefit from Liverpool's loss
24 May, 11:40
International News
Klopp less excited about second final appearance
25 May, 18:48
International News
Don't compare Salah to Messi and Ronaldo, says Ramos. They're in a different orbit!
25 May, 21:14