CAF CC: Gendarmerie kuwasili Jumamosi, Simba watamba kushinda

CAF CC: Gendarmerie kuwasili Jumamosi, Simba watamba kushinda

08 Feb, 19:06

Timu ya soka ya Gendarmerie Nationale ya nchini Djibouti inatarajiwa kuwasili nchini Usiku wa kuamkia Jumamosi kwa ajili ya kucheza na wenyeji timu ya soka ya Simba Sport Club katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Kikosi hicho kinatarajiwa kutua nchini majira ya saa 7:30 usiku wakiwa na msafara wa wachezaji 18 pamoja na viongozi nane, kama ambavyo taarifa ya klabu hiyo ilivyoeleza.

Katika mchezo huo ambao utafanyika Februari 11 Mwamuzi wa kati atakuwa Alier Michael James akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Suleiman Gassim, huku mwamuzi msaidizi namba mbili Gasim Madir Dehiya.

Kadhalika katika mchezo huo mwamuzi wa akiba akiwa ni Kalisto Gumesi Simon Samson na Kamishna wa mchezo huo kutoka Botswana ni Mmonwagotlhe Edwin Senai.

Maandalizi ya mechi.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema maandalizi yote ya mchezo yamekamilika na mgeni rasmi wa mchezo huo ambao utafanyika katika uwanja wa Taifa ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

“Sisi tunamuita mzee wetu mzee mwinyi aje ashuhudie burudani ya mchezo wa mpira wa miguu, hii ni kutokana na kauli yake aliyoitoa mwaka 1988 kuwa Tanzania ni kichwa cha mwenzawazimu kila kinyozi anajifunza kunyolea, japo bado hatujafuta ile kauli wala hatujafika kiwango cha kutamba,” amesema.

Burudani ya mziki

Manara amesema maandalizi hayo yanakwenda sambasamba na kuandaa burudani ya muziki ya kusherehekea kurejea katika kuiwakilisha Taifa kwenye michuano ya kimataifa na burudani hiyo itatolewa kabla ya kuanza kwa pambano hilo.

Kwa upande mwingine Manara amewaomba Mashabiki wote wa Simba kujitokeza na kuanikiza kwa wingi wakiwa na mavazi yanayoonesha upenzi wao kwa timu yao na kwa pamoja kuishangilia Simba ili kupata matokeo mazuri.

Aidha Manara amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo dhidi ya Yanga na St Louis katika michuano ya klabu bingwa Afrika, na kuiunga mkono timu hiyo ili kwa pamoja kuona timu za Tanzania zinafanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Related news
related/article
International News
Ten-man Fulham downs Villa to secure PL return
16 hours ago
International News
Zidane: Madrid not favourites for Champions League final
23 hours ago
International News
CL Final:Liverpool boss expects his side to be brave
26 May, 08:15
International News
UEFA CL: Real Madrid v Liverpool in numbers
25 May, 14:50
International News
Batshuayi puts off Chelsea plans until after World Cup
25 May, 13:50