ASFC: Yanga kwenda Songea, Azam uso kwa uso na wageni wa VPL

ASFC: Yanga kwenda Songea, Azam uso kwa uso na wageni wa VPL

08 Feb, 11:39

Raundi ya nne ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara (Azam Sports Federation Cup) imefanyika asubuhi ya Alhamis ambapo timu 16 zimehusika katika droo hiyo.

Miongoni mwa timu hizo ni ile ya Buseresere FC ambao ni mabingwa wa mkoa wa Geita (Timu pekee ya ligi daraja la tatu) ambao wao wamepangwa kucheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa Kahama uliopo mkoani Shinyanga.

Yanga ambao walikuwa mabingwa wa msimu wa 2015/16 wamepangwa kucheza Wanalizombe timu ya soka ya Majimaji katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Wakati huo huo Kocha Jamhuri Kihwelu Julio atatakiwa kurejea tena mkoani Shinyanga na mara hii amepangwa kucheza na Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage, ikumbukwe katika raundi ya tatu timu ya Dodoma FC inayoongozwa na Julio waliwatoa Mwadui FC.

Ratiba kamili. 

Stand United Vs Dodoma FC - CCM Kambarage, Shinyanga.

JKT Tanzania SC Vs Ndanda FC - Mbweni, Dar.

Kiluvya United Vs Tanzania Prisons - Filbert Bayi, Pwani.

KMC Vs Azam - Uhuru, Dar.

Majimaji Vs Young Africans SC - Majimaji, Ruvuma.

Singida United Vs Polisi Tanzania - Namfua, Singida.

Njombe Mji Vs Mbao FC - Sabasaba, Njombe.

Buseresere FC Vs Mtibwa Sugar - Taifa Kahama, Shinyanga.

Mechi hizo za hatua ya 16 bora zimepangwa kuchezwa Kati ya Februari 22 hadi 25 ambapo washindi watakwenda moja kwa moja katika hatua ya robo fainali na baadae nusu fainali.

Ikumbukwe mpaka sasa hakuna bingwa mtetezi kwani waliokuwa mabingwa Simba SC walitolewa mapema katika hatua ya pili ya mashindano hayo na timu ya Green Warriors ambao nao waliishia mikononi mwa Singida United. Bingwa wa michuano hiyo ataliwakilisha Taifa katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

Related news
related/article
International News
Iniesta unveiled
17 hours ago
Local News
Vipers are 2017-18 Uganda Premier League champions
25 May, 21:05
International News
Ancelotti delighted with return
24 May, 08:55
International News
Great players have to play here - Real Madrid's Marcelo continues Neymar courtship
25 May, 16:18
International News
Ronaldo at '140 per cent' is good enough for Zidane
25 May, 20:54