Zuberi Katwila: Mtibwa hatuko mbali tutarejea mbio za ubingwa

Zuberi Katwila: Mtibwa hatuko mbali tutarejea mbio za ubingwa

08 Feb, 11:10

Kocha Mkuu wa Timu ya Mtibwa Sugar ya kutoka Mkoani Morogoro Zuberi Katwila, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kufuatia matokeo mabaya wamekuwa wakionyesha hivi karibuni na kusema kuwa ni makosa tu ya kawaida ambayo imekuwa ikijitokeza na kuahidi kuyafanyia kazi. 

Akizungumza na futaa.co.tz Katwila amesema kuwa hawajakuwa wakipoteza michezo yao kwa kutojipanga ila ni matokeo ya mpira ambapo wakati mwingine unapata ushindi au kipoteza. "Matarajio yangu ni kufanya vizuri lakini mchezo husika ukifika ukikosa matokeo mazuri unamshukuru Mungu na kusonga mbele, tumepoteza michezo mitatu tutaangalia mbele hatutaangalia hapo tulipojikwaa kwa hio Mwenyezi Mungu anakuangalia na wewe unajilinda", amesema Katwila. 

 Kwa sasa kocha huyo ameahidi kuwekeza nguvu nyingi katika mchezo ujao ili kuimarisha nafasi yao katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara na kufufua matumaini ya kumaliza katika nafasi tatu za juu msimu huu. 

 Mtibwa Sugar ambao hawajapata ushindi kati ya michezo mitano ya hivi karibuni, wanashika nafasi ya 5 wakiwa na alama 33 wakati vinara wa ligi hiyo Simba SC wakiongoza wakiwa na alama 41 Singida United wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama 35 nao Yanga wakifunga tatu bora wakiwa na alama 34. 

 Mtibwa Sugar watacheza na Mbao Fc mchezo ujao utakaofanyika Februari 11, 2018 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mwadui Fc 3- 1 Mtibwa Sugar

Stand United 2 - 1 Mtibwa Sugar

Mbeya City 0 - 0 Mtibwa Sugar

Mtibwa Sugar 0 - 0 Njombe Mji

Lipuli Fc 0 - 1 Mtibwa Sugar

Related news
related/article
International News
WC 2018: Rabiot hits out at France boss
26 May, 09:00
International News
Ronaldo: I can't be compared with Salah
25 May, 14:25
International News
Football legend set to marry two women at same time
24 May, 14:40
International News
Barcelona defender hails Griezmann
26 May, 08:05
International News
Liverpool motivated by Europa League pain - Henderson
25 May, 19:45