CAF CL: St Louis wafanya mazoezi ya kwanza jiji Dar

CAF CL: St Louis wafanya mazoezi ya kwanza jiji Dar

07 Feb, 20:46

Klabu ya soka ya St. Louis kutoka Ushelisheli imefanya mazoezi ya kwanza ndani ya jiji la Dar es Salaam tayari kukipiga na klabu ya Dar Young Africans katika hatua ya awali ya Ligi ya mabingwa barani Afrika.

St Louis waliwasili usiku wa kuamkia Jumatano ya Februari 7 na wamefanya mazoezi hayo katika uwanja wa Karume mapema asubuhi.

Saint Louis imetokea wapi?

Ni klabu yenye makao yake makuu kwenye jimbo la Victoria nchini Shelisheli, imezaliwa mwaka 2007 baada ya muungano wa timu 2 yaani Saint-Louis (iliyoundwa mwaka 1985) na Sunshine (iliyokuwepo toka mwaka 199 ).

Mwishoni mwa mwaka jana walitawazwa rasmi kama Mabingwa wa ligi kuu nchini humo, wakiwa wametwaa pia Kombe la shirikisho msimu huo huo.

Kikosi cha St Louis Suns United kina jumla ya wachezaji 18, wachezaji watatu tu wanaotokea nje ya nchi hiyo, kwa idadi ya kiungo mmoja kutoka Nigeria na wengine wawili kutoka Cape Verde.

Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia na Kamishna wa mchezo akitokea nchini Namibia.

Waamuzi

Mwamuzi wa kati atakuwa Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Gizaw Belachew na mwamuzi msaidizi namba mbili Kinfe Yilma Kinfe wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Amanuel Heleselass Worku na Kamishna Frans Vatileni Mbidi.

Ikumbukwe mchezo kati ya Yanga na St Louis unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi Februari 10, mwaka huu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kama Yanga watafanikiwa kufudhu katika hatua hiyo watakutana na Mshindi wa mchezo kati ya Township Rolers ya Botswana au Merrikh ya Sudan.

Related news
related/article
International News
Barcelona defender hails Griezmann
26 May, 08:05
International News
UEFA CL: Real Madrid v Liverpool the key battles
25 May, 17:00
International News
REVEALED: Why Iniesta chose Japan
24 May, 13:50
International News
Klopp less excited about second final appearance
25 May, 18:48
International News
No offers for Lyon captain Fekir, Aulas claims
25 May, 21:57