VPL: Vikosi vya Mbao, Singida Utd vyawekwa wazi

VPL: Vikosi vya Mbao, Singida Utd vyawekwa wazi

07 Feb, 14:05

Kocha Etienne Ndairagije wa kikosi cha timu ya soka ya Mbao FC amemuanzisha benchi mshambuliaji Emmanuel Mvuyekule katika mchezo wa ligi dhidi ya Singida United.

Katika mchezo huo ambao utafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Habibu Kiyombo ambaye anaongoza kwa mabao katika kikosi cha Mbao akiwa na mabao 8 ameanza pamoja na James Msuva ambao ndio watakaoongoza mashambulizi.

Aidha kipa Matacha Mnata ameendelea kuaminika baada ya kuonesha mchezo mzuri katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar, amechaguliwa kuanza tena akimuweka benchi Yvan Rugumandiye.

Kinachoanza: Matacha Mnata 33, Vincent Philipo 9, Amos Abel 25, David Mwasa 4, Yusuph Ndikumana 14, Ibrahim Njohole 22, Abubakar Ngalema 19, Hussein Kasanga 8, Habibu Haji Kiyombo 17, Ismail Ally 7, James Msuva 13.

Akiba: Yvan Rugumandiye 1, Ally Kombo 6, Emmanuel Mvuyekule 10, Said Khamis 3, Abdulkarim Segeja 2, Seleman Bwelle 29 na Herbert Lukindo 22.

Singida United 

Kwa upande wa wageni Singida United golini ataendelea kuwepo mkongwe Ally Mustapha 'Barthez' badala ya Manyika Jr ambaye hajapangwa toka walipopoteza 4-0 dhidi ya Simba.

Kadhalika nahodha wa zamani wa Toto Africans Salumu Chuku amepangwa kuanza kwenye mchezo huo, na alionesha mchezo mzuri wakati Singida waliposhinda 3-2 dhidi ya Mwadui Wikiend iliyopita.

Kinachoanza: Ally Mustapha 30, Michael Rusheshangonga 22, Shafik Batambuze 6, Malik Antiri 3, Salum Kipaga 5, Mudathir Yahya 27, Deus Kaseke 7, Yusuf Kagoma 21, Lubinda Mundia 11, Kenny Ally 8 na Salumu Chuku 12.

Akiba Said Lubawa 1, Miraji Adam 24, Kiggy Makasi 4, Mohamed Abdallah 26, Assad Juma 13, Ally Ng'anzi na Tafadzwa Kutinyu 20.

Related news
related/article
International News
Luiz: Salah can win Ballon d'Or with Champions League triumph
22 hours ago
International News
Pochettino signs new deal with Tottenham
25 May, 08:10
International News
UEFA CL: Road to Kiev
23 May, 19:00
International News
FA condemns assault of match official
24 May, 20:18
International News
Lyon win record fifth Women's Champions League title
24 May, 22:47