Kabange: Huu sio muda wa kukata tamaa

Kabange: Huu sio muda wa kukata tamaa

06 Feb, 20:04

Kocha mkuu wa Kikosi cha soka cha Njombe Mji Mrage Kabange amesema bado wamebakiwa na mechi nyingi ambazo zinaweza kuwaonesha njia yao kama watashuka daraja au laa.

Kabange ambaye ni winga wa zamani wa Simba na kocha wa vilabu kadhaa kikiwemo Kagera Sugar amesema mashabiki wanapaswa kuhuzunika lakini si kukata tamaa kutokana na matokeo wanayoendelea kuyapata.

"Tuna mechi kama 13 hivi kwa maana bado tuna nafasi ya kuweza kujitetea na kuangalia wapi timu itakapofika, kwa hatupaswi kukata tamaa tunaweza kupambana," amesema.

Kabange ambaye ameiongoza Njombe Mji toka kuondoka kwa kocha Hassan Banyayi mwanzoni mwa msimu amesema hata yeye anashindwa kuelewa ni wapi wanakosea kwani makosa wanayofanya kila siku huwa yanajirudia.

Makosa ni madogo  

"Makosa ndo kama hayo yanatokea kila siku, makosa madogo madogo ndo yanatugharimu, wenzetu wanatumia, tutaendelea kuyafanyia kazi haya makosa ili yasiendelee kutokea," Kabange amesema.

Njombe Mji wamekubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Dar Young Africans katika mchezo wa ligi uliofanyika Februari 6 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Njombe Mji mpaka sasa ndio inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 13 huku tayari wakiwa wamecheza michezo 17.

Related news
related/article
International News
Arsenal bump up Emery's transfer budget
1 hour ago
Transfer News
Transfer Talk: Midfielder signs permanent deal with Valencia
24 May, 15:20
International News
Rwanda to sponsor Arsenal's new sleeve
23 May, 11:05
International News
Football legend set to marry two women at same time
24 May, 14:40
Transfer News
Transfer Talk: Villareal midfielder completes move to Atletico Madrid
24 May, 15:50