Vikosi vinavyoanza kwenye mchezo wa Yanga na Njombe Mji, Beno arejea kikosini

Vikosi vinavyoanza kwenye mchezo wa Yanga na Njombe Mji, Beno arejea kikosini

06 Feb, 13:51

Kipa Beno Kakolanya amerejea kikosini na mara hii ameanzia benchi katika kikosi cha Dar Young Africans kitakachocheza na Njombe Mji jioni hii kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kakolanya ambaye stori yake imegubikwa na migomo ya kudai malipo yake, amepangwa kuanzia benchi wakati uwanjani akiwepo kinda Ramadhan Kabwili ambaye alidaka vyema mchezo uliopita dhidi ya Lipuli baada ya kuumia kwa Youthe Rostand.

Katika kikosi hicho Makka Edward ambaye mchezo uliopita aliingia akitokea benchi ameanza wakati Juma Mahadhi ambaye alicheza vizuri kwenye michuano ya mapinduzi Cup akianzia benchi.

Kinachoanza: Ramdhani Kabwili, Gadiel Michael, Hassan Kessy, Kelvin Yondani, Juma Makapu, Maka Edward, Pius Buswita, Papy kabamba, Obrey Chirwa, Raphael Daud na Emmanuel Martin.

Akiba: Beno Kakolanya, Said Musa, Yusuf Mhilu, Buruan Akilimali, Juma Mahadhi na Matheo Anthony.

Njombe Mji. 

Kwa upande wa wapinzani wao Njombe Mji wanaingia katika mchezo huo wakiwa na wakimataifa wawili ambao wamepangwa katika kikosi kinachoanza.

Heririmana Lewis na Etienne Ngiladjoe wameanza pamoja na mchezaji aliyewaniwa sana na Yanga katika dirisha dogo la usajili Ditram Nchimbi.

Kinachoanza: Rajabu Mbululu, Agathon Mapunda, Harerimana Lewis, Ahmed Adewale, Raban Kambole, Aden Chepa, Willy Mgaya, Juma Mpakala, Etienne Ngiladjoe, Ditram Nchimbi na Claide Wigenge.

Akiba: David Kissu, John Sagala, Mack Mwambungulu, Jimmy Mwasongola, Raphael Siame, David Obash na Nickson Kibabage.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0, likifungwa na Ibrahim Ajib kwa faulo ya moja kwa moja, mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Related news
related/article
International News
Iniesta's Vissel Kobe move confirmed
24 May, 11:35
International News
Ancelotti delighted with return
24 May, 08:55
International News
UEFA Champions League final: Key players
23 May, 16:00
International News
Buffon in consideration for Italy call, says Mancini
24 May, 16:10
International News
Spalletti in 'no rush' to sign new Inter deal
24 May, 19:31