Venance Kazungu: Bado ni vigumu kutabiri mshindi kundi C

Venance Kazungu: Bado ni vigumu kutabiri mshindi kundi C

12 Jan 2018, 18:45

Kocha Mkuu wa Timu ya Pamba inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza Tanzania Bara 'FDL' Venance Kazungu, amesema kuwa lengo lake ni kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo iliyobaki ili kumaliza ligi katika nafasi nzuri msimu huu.

Akizungumza na futaa.co.tz  kuhusu mchezo wao dhidi ya Transit Camp ya kutoka mkoani Shinyanga, Kazungu amesema kuwa anaendelea  kuwaandaa vijana vizuri ili kuhakikisha wanapata ushindi na kuimarisha nafasi yao ya kufanya vizuri.

Hata hivyo Kazungu amesema kundi lao la  C lina ushindani mkubwa na kuwa kufikia sasa hawawezi wakatabiri nani atamaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili.

-Tulianza mazoezi Jumatatu kwa maandalizi kati yetu na Transit Camp, haja sio tu kuleta ushindani ila tunataka kushinda mechi hii ili kuiweka timu yetu katika nafasi nzuri, hatujapoteza sana kwani mechi hizi za mwisho huwezi ukajua nani anaweza akachukua nafasi ya kwanza na ya pili kwa hiyo tumejiweka vizuri kwa ajili ya mchezo huo, amesema Kazungu.

Kuhusu hali ya wachezaji kukabiliana na ugumu wa ligi kufuatia madai ya fitina kwa baadhi ya timu  Kazungu amesema kuwa wameshawaandaa wachezaji kisaikolojia kukabiliana na matukio ya aina hio na hivyo hilo si tatizo wao kufanya vibaya. 

-Mchezo wa biashara wachezaji waliona ni jambo la kawaida kwa sababu kuonewa au kutoonewa tumeshawajenga kisaikolojia kwamba kwenye mpira hayo yote yapo kwa hio wakubali yote kwa aina yoyote itakayoyokea ili wasijitoe kwenye mpira na kuanza vurugu", amesema Kazungu. 

Ukata unawasumbua.

Pamoja na hayo Kazungu amekiri uhaba wa fedha za maandalizi umekuwa ukiwatatiza na kushindwa kuandaa mechi nyingi za kirafiki kama vile wangependa ili kuimarisha mchezo wao.  

Pamba Fc ambao wako kundi C wanashika nafasi ya 5 katika msimamo wa kundi hilo wakiwa na alama 12 Wakati Transit Camp wakishika nafasi ya 7 wakiwa na alama 10.

Related news
related/article
FIFA World Cup
Delph: We already know England's XI for Tunisia tie
16 Jun 2018, 18:15
International News
BREAKING: Arsenal ace pens new long-term contract
12 Jun 2018, 16:35
Transfer News
Transfer Talk: Barca identifies Iniesta replacement, United hits brick wall in defender's pursuit
17 Jun 2018, 12:20
Transfer News
West Ham confident of signing Arsenal midfielder
18 hours ago
FIFA World Cup
Gareth Southgate hails England show
10 hours ago