Mapinduzi Cup: Azam kuwafanyia mazoezi mepesi URA

Mapinduzi Cup: Azam kuwafanyia mazoezi mepesi URA

11 Jan 2018, 19:12

Kikosi cha Wanarambaramba Azam FC kimepewa mapumziko mafupi ya siku moja kabla ya Ijumaa kurejea tena katika mazoezi mepesi kujiandaa na mchezo wa fainali wa Mapinduzi Cup dhidi ya URA ya Uganda Jumamosi ya Januari 13.

Kocha msaidizi wa Azam Seleman Idd Cheche amesema benchi la ufundi kwa pamoja wameshauriana na kuona ni vizuri wachezaji wote wakapewa mapumziko lakini pia wafanye mazoezi mepesi kabla ya kuvaa na URA.

Amesema walifanya hivyo baada ya kutinga hatua ya nusu fainali na iliwasaidia kwani waliweza kuwatoa Singida United katika mchezo wa nusu fainali kwa kuwafunga 1-0 bao ambalo liliwekwa kimiani na Kinda Shaban Idd Chilunda.

-Wachezaji wanapumzika kidogo, kwani haikuwa kazi rahisi tumetumia nguvu nyingi, na hata mazoezi tutafanya mepesi ili kupata recovery kwa sababu michezo ilikuwa karibu karibu sana, amesema.

Azam wanakutana na URA katika mchezo wa fainali, timu ambayo iliwafunga kwa bao 1-0 katika mchezo wa kundi A, kitu ambacho Cheche anasema anaamini itakuwa tofauti kwani watajiandaa vizuri tofauti na mchezo huo wa hatua ya makundi.

-Mchezo wa fainali ni tofauti, utakuwa mchezo wa ushindani na mgumu, tuliwahi kukutana nao kwenye pre season na tuliwafunga na wao wakatufunga kwenye mchezo wa makundi, kwa hiyo ni watu ambao kwa kiasi Fulani tunajuana na mapambano yatakuwa ni makali, Cheche ameongeza.

Taji la nne.

Mchezo huo wa fainali utafanyika kuanzia majira ya saa 2:15 usiku ambapo kama Azam wataibuka na ushindi basi watakuwa wamejiwekea historia ya kwao wenyewe ya kutetea taji hilo kwani waliwahi kufanya hivyo mwaka 2012 na 2013.

Mwaka 2012 Azam waliingia fainali na kuifunga Jamhuri Pemba kwa mabao 3-1 wakati mwaka 2013 walichukua taji kwa kuichapa Tusker FC ya Kenya mabao 2-1.

Kwa Upande wa URA kama watafanikiwa kutwaa taji, litakuwa ni taji la pili baada ya lile walilolitwaa mwaka 2016 kwa kuwafunga wakata miwa wa Turiani mkoani Morogoro Mtibwa Sugar kwa mabao 3-1.

Related news
related/article
International News
Neymar downplays his €222m price tag
14 Jun 2018, 18:35
FIFA World Cup
WC 2018: Four teams that could spring a surprise in Russia
13 Jun 2018, 20:00
International News
Mihaljovic joins problematic Sporting
2 hours ago
FIFA World Cup
Neymar misses Brazil training
14 hours ago
FIFA World Cup
What went wrong for Brazil?
21 hours ago