Matola amegoma? Lipuli watoa ufafanuzi

Matola amegoma? Lipuli watoa ufafanuzi

11 Jan 2018, 17:39

Uongozi wa klabu ya soka ya Lipuli ya mkoani Iringa umesema utatolea ufafanuzi hivi karibuni kuhusiana na suala la kocha wake msaidizi Seleman Matola kudaiwa kugoma kuifundisha timu yao baada ya kutofautiana kauli na kocha mkuu Amri Said.

Lipuli kupitia Afisa wake wa habari Clement Sanga imesema hawawezi kutoa ufafanuzi kuhusiana na jambo hilo kwa sasa na kuomba subira pale watakapokuwa tayari basi wataweza kutoa ufafanuzi.

-Kwa sasa hilo naomba tuliache na tuliweke pembeni, nitalitolea ufafanuzi pale nitakapokuwa vizuri kwa ajili ya Public Consumption basi nitakujuza, ila kwa hatua tuliyofikia sasa atakuwepo tu msiwe na wasiwasi, Sanga amesema.

Kikao cha kamati tendaji

Awali kulikuwa na taarifa ya kufanyika kikao cha kamati tendaji hapo Januari 10, kikao ambacho kinasemekana kuleta ugomvi na kutoelewana baina ya Matola na Amri Said jambo ambalo lilimfanya Matola kugomea kufundisha timu hiyo.

Kadhalika kulikuwa na taarifa ya kocha Matola kutakiwa na wekundu wa msimbazi ili akawe kocha msaidizi katika kikosi hicho ambacho mpaka sasa kimekuwa na matokeo yasiyoridhisha.

Related news
related/article
FIFA World Cup
Late Uruguay goal crushes Egypt
15 Jun 2018, 16:55
International News
CAF turns down idea to pair World Cup 2022, AFCON 2021 qualifiers
12 Jun 2018, 12:15
International News
Wolves sign Portugal international
3 hours ago
FIFA World Cup
Mini-earthquake reported in Mexico due to celebrations
17 Jun 2018, 21:00
FIFA World Cup
Harry Kane the hero, as England stab resilient Tunisia
11 hours ago