Bilal: Nina furaha kurejea tena kazini

Bilal: Nina furaha kurejea tena kazini

11 Jan 2018, 17:08

Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Stand United Athumani Bilal ‘Bilo’ amesema anafurahi kurejea kazini baada ya kusimamishwa kwa muda mfupi kutokana na kile ambacho uongozi wa klabu hiyo kusema kuwa ni utovu wa nidhamu.

Bilal amesema lilikuwa ni jambo dogo na ndio maana uongozi wa klabu hiyo umemfikiria upya na kuamua kumrejesha kazini na yeye anatambua thamani hiyo hivyo kazi kubwa anayoona kapewa ni kuisaidia timu hiyo kutoka mkiani ilipo hivi sasa.

-Nasema kusimamishwa ni changamoto za kazi na changamoto humpata mwanadamu, uongozi umekaa umefikiria na kuona nafaa kurejea tena kazini, na akili yangu kubwa sana kwa sasa ni kuitoa Stand United sehemu ilipo na kuipeleka sehemu yenye usalama zaidi, Bilal amesema.

Ahadi kubwa ambayo kocha Bilo ameitoa ni ushirikiano baina yake na uongozi pamoja na kocha mkuu Ramadhan Nswazurimo ili kuweza kuisaidia timu hiyo kufika malengo yake.

Kocha huyo ambaye amewahi pia kuifundisha timu ya soka ya Toto Africans ya Mwanza amesema atahakikisha anatimiza anatimiza malengo yote waliyowekeana na uongozi ikiwemo kufanya vizuri katika michuano ya kombe la shirikisho.

-Msimu uliopita Stand tulimaliza nafasi ya sita, na mwanzoni mwa msimu tuliweka mipango ya angalau kuwa katika nafasi ya nne, hatujafanya vizuri hilo linaukweli lakini bado hatujachelewa, mimi nina uhakika kabisa tutafanya vizuri, amesema.

Ruvu Shooting

Kuhusiana na mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting utakaofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage Januari 13, Bilal amesema wamejiandaa vizuri ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa mwaka jana uongozi wa Stand United ulimsimamisha kocha huyo kwa kosa la utovu wa nidhamu

Aidha Uongozi huo umeamua kumrejesha baada ya kuzungumza kwa kina kuhusiana na hilo na moja ya masharti aliyopewa ni kuhakikisha harudii kosa lake la utovu wa nidhamu kwani mpaka sasa ni mara ya pili anaadhibiwa kwa kosa hilo.

Related news
related/article
International News
China tipped to be 'super power' in world football
15 Jun 2018, 15:50
FIFA World Cup
Group B Preview - Spain and Portugal set to crash Morocco's hopes
11 Jun 2018, 15:50
FIFA World Cup
Neymar misses Brazil training
14 hours ago
FIFA World Cup
World Cup over for Croatia striker
14 hours ago
International News
Arsene Wenger praises Kante
20 hours ago