Kiyombo amwangusha Bocco na kutwaa tuzo ya mwezi Disemba

Kiyombo amwangusha Bocco na kutwaa tuzo ya mwezi Disemba

11 Jan 2018, 15:17

Mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo amechaguliwa Mchezaji Bora wa mwezi Disemba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2017/2018.

Kiyombo ameibuka mchezaji bora baada ya kuwashinda wachezaji wenzake wawili alioingia nao fainali kutokana na tathmini iliyofanywa na kikao cha Kamati ya Tuzo wiki hii.

Kwa mwezi Disemba ambao timu 12 kati ya 16 zinazoshiriki ligi hiyo kila moja ilicheza mechi moja, Kiyombo aliisaidia timu yake kufunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Yanga ambao Mbao ilishinda mabao 2-0.

Kutokana na matokeo hayo, Mbao ilipanda kutoka nafasi ya nane hadi ya saba katika msimamo wa ligi, huku Kiyombo akifikisha mabao saba ya kufunga kwake msimu huu, akiwa nyuma ya Emmanuel Okwi wa Simba anayeongoza akiwa na mabao nane.

Aliowashinda 

Kiyombo aliwashinda mshambuliaji wa Simba, John Bocco aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 2-0 wa Simba dhidi ya Ndanda na beki Bruce Kangwa aliyeisaidia Azam katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United.

Katika mchezo huo wa Azam, beki huyo alifunga bao moja na kutoa pasi ya usaidizi wa bao lingine. Wachezaji wote hao hakuna aliyepata kadi.

Kutokana na ushindi huo, Kiyombo atazawadiwa tuzo, kisimbusi cha Azam na fedha taslimu shilingi 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wakuu wa Ligi hiyo, Kampuni ya Vodacom.

Waliotwaa tuzo msimu huu. 

Wachezaji wengine ambao tayari wametwaa tuzo ya mwezi kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi (Agosti), Shafiq Batambuze (Septemba), Obrey Chirwa (Oktoba) na Mudathir Yahya( Novemba).

Related news
related/article
Transfer News
West Ham confident of signing Arsenal midfielder
17 hours ago
FIFA World Cup
Brazil warned ahead of Switzerland clash
15 Jun 2018, 10:35
International News
Wolves sign Portugal international
3 hours ago
FIFA World Cup
Neymar misses Brazil training
14 hours ago
International News
Salah to face fitness test
11 hours ago