CECAFA 2017: Ninje akosa namna, aamua kuwavulia kofia Zanzibar

CECAFA 2017: Ninje akosa namna, aamua kuwavulia kofia Zanzibar

07 Dec 2017, 20:49

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya soka ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ Ammy Conrad Ninje amesema sababu kubwa iliyowafanya kupoteza mchezo dhidi ya ndugu zao Zanzibar kwa mabao 2-1, katika michuano ya CECAFA ni wachezaji wake kukosa kujitambua na kujituma.

Amesema timu zote mbili zilicheza vizuri lakini timu yake ilizidiwa eneo hilo ambapo kama wachezaji wake wangeonesha hali ya kujituma toka mwanzo wangeshinda mchezo huo kwani tayari walikuwa wanaongoza mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

-Tulianza vizuri kipindi cha kwanza tulicheza vizuri sana, lakini kipindi cha pili tulikuwa hovyo, Zanzibar walionekana kuhitaji matokeo zaidi kuliko sisi, wamecheza kwa moyo na kujituma kwa kipindi cha pili lakini sio kwa kucheza mpira mzuri, na ndio maana wameshinda mchezo huu, amesema.

Ninje amesema hana budi kumpongeza kocha wa Zanzibar Hemed Suleiman Morocco kwa kukijenga kikosi chake vizuri na katika hali hiyo wameonesha nia zaidi ya kushinda tofauti na ilivyokuwa kwao na ndio maana wameshinda mchezo huo.

-Wao wanastahili kuchukua pointi hizi tatu katika mchezo huu, kwa hiyo nampongeza mwalimu wao kwa juhudi walizozifanya, matayarisho yao yalikuwa magumu lakini wameonesha kwamba kwenye mpira ukiwa na nia ya kitu chochote na ukakifanya kwa moyo unaweza kufanikiwa, Ninje amesema.

Nafasi ya Kili Stars.

Katika mchezo huo wa Kundi A licha ya Kilimanjaro Stars kutangulia kwa bao 1 ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Himid Mao, lakini walijikuta wakipoteza kwa mabao 2-1 baada ya wachezaji Kassim Suleiman na Ibrahim Hamad Ilika kufunga katika kipindi cha pili.

Kilimanjaro Stars wamebakiwa na michezo miwili dhidi ya Rwanda na wenyeji Kenya kukamilisha michezo ya hatua ya makundi, ambapo kama watashinda michezo yote watafikisha alama 7.

Related news
related/article
FIFA World Cup
Keane blasts England defender
12 Jul 2018, 12:35
FIFA World Cup
Croatia keeper to play through injury
10 Jul 2018, 16:55
FIFA World Cup
Ibrahimovic hails Pogba
3 hours ago
FIFA World Cup
Courtois wins World Cup Golden Glove award
14 hours ago
Ligue 1
Buffon beaten on PSG debut
20 hours ago