CECAFA 2017: Mudathir, MO Banka waanza pambano dhidi ya Kili Stars.

CECAFA 2017: Mudathir, MO Banka waanza pambano dhidi ya Kili Stars.

07 Dec 2017, 11:30

Viungo pacha Mudathir Yahya na Mohamed Issa Rashid wameanza pamoja katika kikosi cha Zanzibar kitakachopambana na Tanzania Bara katika muendelezo wa michuano inayosimamiwa na Baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati 'CECAFA'.

Katika kikosi hicho kilichopangwa na Kocha Hemed Suleiman Morocco, mfungaji wa bao la tatu katika mchezo uliopita dhidi ya Rwanda Khamis Mussa, ameanzia benchi pamoja na mlinzi wa kati wa Dar Young Africans Abdalah Shaibu 'Ninja'.

Zanzibar Heroes watajitupa uwanjani kuwakaribisha Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' katika mchezo wa Kundi A utakaofanyika kwenye uwanja wa Kenyatta uliopo Kaunti ya Machakos nchini Kenya, mchezo unaotarajiwa kuanza majira ya saa 8 mchana.

Kikosi kitakachoanza na namba zao mgongoni. 

1. Mohamed Abrahman (Wawesha) 18.

2. Ibrahim Mohamed (Sangula) 15.

3. Haji Mwinyi Ngwali 16.

4. Abdulla Kheri (Sebo) 13.

5. Issa Haidar Dau (Mwalala) 8.

6. Abdul azizi Makame (Abui) 21.

7. Mohamed Issa (Banka) 10.

8. Mudathir Yahya 4 (Captain).

9. Ibrahim Hamad Hilika 17.

10. Feisal Salum (Fei Toto) 3.

11. Hamad Mshamata 9.

Wachezaji wa akiba. 

1. Ahmed Ali (Salula) 1.

2. Ibrahim Abdallah 2.

3. Adeyum Saleh 20.

4. Abdullah Haji (Ninja) 5.

5. Seif Rashid (Karihe) 12.

6. Kassim Suleiman 19.

7. Suleiman Kassim “Seleembe” 7.

8. Khamis Mussa (Rais) 28.

9. Amour Suleiman (Pwina) 14.

10. Abdul swamad Kassim (Hasgut) 22

Related news
related/article
English Premier League
Courtois responds to Real Madrid links
15 Jul 2018, 08:55
FIFA World Cup
Ex-England boss hails Pickford
10 Jul 2018, 17:15
Seria A
Ronaldo's Juve move defended
1 hour ago
FIFA World Cup
Courtois wins World Cup Golden Glove award
14 hours ago
FIFA World Cup
Luka Modric bags the World Cup Golden Ball award
15 hours ago