CECAFA 2017: Ajib nje, Maguri Kichuya waanza pambano dhidi ya Zanzibar Heroes

CECAFA 2017: Ajib nje, Maguri Kichuya waanza pambano dhidi ya Zanzibar Heroes

07 Dec 2017, 11:21

Kocha Ammy Conrad Ninje amemuanzisha Mshambualiaji mpya wa Polokwame City ya Afrika Kusini Elius Maguri katika kikosi cha Tanzania Bara kitakachopambana na timu ya Zanzibar kwenye muendelezo wa michuano inayosimamiwa na Baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati 'CECAFA'.

Maguri ambaye alianza katika mchezo dhidi ya Libya uliomalizika kwa sare ya 0-0, atasaidiwa na Daniel Lyanga pamoja na Shizya Kichuya ambao watacheza winga ya kulia na kushoto.

Aidha nahodha wa Kilimanjaro Stars Himid Mao Mkami ameanzishwa katika kikosi hicho ambapo atacheza sambamba na kiungo wa SoNy Sugar Abdallah Hamis pamoja na Mzamiru Yassin katika safu hiyo.

Kikosi kitakachoanza.

1. Aishi Manula.

2. Erasto Nyoni.

3. Gadiel Michael.

4. Kennedy Juma.

5. Kelvin Yondani.

6. Abdallah Hamis.

7.Shiza Kichuya.

8 Himid Mao.

9.Elias Maguri.

10. Daniel Lyanga.

11. Mzamiru Yassin.

Wachezaji wa akiba.

1. Peter Manyika.

2. Boniphace Maganga.

3. Mohammed Hussein.

4. Jonas Mkude.

5. Raphael Daud.

6. Ibrahim Ajib.

7. Abdul Hassan.

8. Yahya Zaydi.

9. Yohana Mkomola.

10. Mbaraka Yussuf.

Related news
related/article
FIFA World Cup
Pogba responds to critics
12 Jul 2018, 07:35
FIFA World Cup
Pickford responds to Courtois criticism
09 Jul 2018, 11:30
Seria A
Ronaldo's Juve move defended
1 hour ago
FIFA World Cup
Ibrahimovic hails Pogba
3 hours ago
English Premier League
BREAKING: Jorginho joins Chelsea
14 Jul 2018, 14:10