CECAFA 2017: Ninje awahofia Zanzibar kutumia mfumo huu

CECAFA 2017: Ninje awahofia Zanzibar kutumia mfumo huu

07 Dec 2017, 08:00

Kocha Mkuu wa kikosi cha timu ya Tanzania bara' Kilimanjaro Stars' Ammy Conrad Ninje, amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya ndugu zao Zanzibar Heroes',katika  michuano ya CECAFA inayoendelea nchini Kenya. 

 Akizungumza na mtandao huu Ninje amesema kuwa anatarajia mchezo wa upinzani lakini hawataukabili kwa staili hiyo ilavya utulivu.

 -Mechi itakuwa ngumu haijawahi kuwa mechi rahisi kati ya Tanzania Bara na Visiwani, ni mchezo wa ushindani lakini mimi nimekuja kwenye angle tofauti nimewaambia wachezaji wangu wa relax sababu zanzibar wana pointi tatu sisi tuna moja tucheze mpira bila emotions tucheze kwa proffessionalism", amesema Ninje. 

 Kwa upande wake Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni pia ameutaja mchezo huo kuwa mgumu huku akiwahofia Zanzibar na kusema umakini utahitajika ili kuwakabili ndugu zao. 

 -Mchezo utakuwa sio rahisi kwanza wachezaji wote tunajuana ,mara zote tumekutana mechi imekuwa ngumu mechi tatu za hivi karibuni wametushinda mbili tunaomba Mungu tushinde mchezo wa Alhamisi", amesema Nyoni.

 Mchezo huo ambao utaanza saa 8.00 utafanyika kwenye uwanja wa Kenyatta uliopo mjini Machakos nchini Kenya. 

Kenya wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 4 , Zanzibar wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama tatu,Libya wako katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 2,Tanzania nafasi ya 4 wakiwa na alama 1 nao Rwanda. Wakivuta mkia wa kundi hilo bila pointi yeyote.  

Ratiba 07/12/2017

Tanzania - Zanzibar 8.00 Machakos 

 Libya - Rwanda 10.00 Machakos 

 Ethiopia- Burundi 9.00 Bukhungu

Related news
related/article
English Premier League
Kane hopes to break August curse
2 hours ago
English Premier League
Conte out: Sarri's training methods examined
13 Jul 2018, 13:50
FIFA World Cup
France defender retires from international football
3 hours ago
FIFA World Cup
Hazard speculates his future
16 hours ago
Transfer News
Ronaldo was open to Napoli move
20 hours ago