Mrithi wa Yahaya Mohamed, rada za Azam zaangukia Zambia na Ghana.

Mrithi wa Yahaya Mohamed, rada za Azam zaangukia Zambia na Ghana.

14 Nov 2017, 18:44

Ikiwa imepita juma moja toka Klabu ya Azam ‘Wanarambaramb’ ya jijini Dar es Salaam kutangaza kuachana na mshambuliaji Yahaya Mohamed, tayari uongozi wa klabu hiyo umethibitisha kuwawinda nyota wawili kutoka mataifa ya Ghana na Zambia kuziba pengo hilo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Afisa habari wa Klabu hiyo Jaffary Idd Maganga amesema tayari rada zao zimewanasa wachezaji wawili ambao muda wowote kutoka hivi sasa watamtangaza mmoja ambaye atakuwa ameliridhisha benchi la ufundi.

Amesema majina ya wachezaji hao yamependekezwa na Kocha Aristica Cioaba na tayari jopo la wataalamu lipo kujadili nani wa kumsajili kati ya hao wawili na ikiwezekana aweze kusainiwa mapema bila kufanyiwa majaribio.

-Tumekuwa na kikao na Mwalimu na alitoa option ya wachezaji wawili kutoka mataifa tofauti ambao ameona wakija wanaweza kumsaidia katika nafasi hiyo ya ushambuliaji, so far hatuwezi kutaja majina lakini nchi wanazotoka ni Zambia na Ghana, sio wachezaji ambao utawaleta uje uwaangalie, akija anakuja kufanya kazi yake,” Amesema Maganga.

Ujumbe umetumwa.

Tayari mjumbe wa Klabu hiyo ameandaliwa kwenda kufanya mazungumzo na wachezaji hao ambao kama mambo yatakuwa mazuri basi wanaweza kusajiliwa katika kipindi kisichozidi juma moja na nusu kutoka leo.

Katika upepelezi ambao mtandao huu umeufanya umefanikiwa kupata jina la mchezaji mmoja kutoka Zambia ambaye anachezea klabu ya Lusaka Dynamos Chrispin Mugalu, ambaye katika msimu huu amefanikiwa kufunga mabao 17 na kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo.

Mechi dhidi ya Njombe.

Katika hatua nyingine Azam FC inatarajiwa kuondoka mapema siku ya Jumatano kuelekea mkoani Njombe tayari kwa maandalizi ya mwishomwisho kuelekea kwenye mchezo wao dhidi Njombe Mji utakaofanyika Novemba 18 katika uwanja Sabasaba.

Maganga ameuambia mtandao huu kuwa jumla ya wachezaji 22 pamoja na benchi la ufundi na viongozi wa klabu hiyo watasafiri, lengo likiwa ni kuwahi na kuweka kambi mapema ili kuzoea mazingira na hali ngumu ya hewa ya mkoa huo.

-Tutamkosa Raphael Bryson ambaye ni majeruhi, lakini kiungo Stephan Mpondo atakuwa miongoni mwa hao wachezaji 22 baada ya kupona majeraha yake, matumaini yetu ni kuwa tutashinda mchezo huo na kuendelea kukaa katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi,” Maganga amesema.

Related news
related/article
FIFA World Cup
France vs Croatia: Road to the Final
22 hours ago
FIFA World Cup
Hazard hails Mbappe
09 Jul 2018, 12:35
English Premier League
Kane hopes to break August curse
2 hours ago
FIFA World Cup
Russia passes on the World cup mantle to Qatar
3 hours ago
Transfer News
Ronaldo was open to Napoli move
20 hours ago