Ligi Kuu: Mbao waitahadhalisha Mbeya City.

Ligi Kuu: Mbao waitahadhalisha Mbeya City.

12 Oct 2017, 20:40

Kocha Mrundi Etienne Ndairagije anayekinoa kikosi cha Mbao FC amesema wiki moja aliyoipata katika maandalizi ya ligi imetosha kabisa kukisuka kikosi chake.

Ndairagije ameyasema hayo wakati akizungumza na mtandao huu mara Baada ya mazoezi ya leo jioni wakijiandaa na mchezo wa Mzunguko wa kwanza,raundi ya Sita dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Ijumaa.

-Tupo vizuri hatuna shida yoyote maandalizi, tumejiandaa vizuri, tumepata wiki moja, Tumejaribu kuweka sawa mambo ambayo yalikuwa hayapo sawa".

Kuhusu Majeruhi?

-Mpaka sasa tunashukuru Mungu hakuna majeraha yoyote kwa wachezaji, tunazidi kumuomba Mwenyezi Mungu atupatie mechi nzuri ili tuweze kupata pointi tatu," Ndairagije ameeleza.

Kwa upande wake nahodha wa Mbao FC Yussuf Ndikumana amesema wanategemea kupata ushindi katika mchezo na wanaomba wavune pointi tatu.

-Matarajio yetu ni kupata pointi tatu, Lakini pia tumejiandaa vizuri, wapinzani wetu tunawaheshimu Kwa sababu ni timu ambayo ipo kwenye ligi Kuu, ila tunatarajia ushindi," Ndikumana amesema.

Rekodi ya mchezo huo. 

Mbeya City FC inaingia katika mchezo huo ikiwa na rekodi ya kuifunga Mbao FC katika michezo yote ya nyumbani na ugenini msimu uliopita.

Mchezo wa kwanza uliochezwa CCM Kirumba Mbeya City FC iliibuka na ushindi wa magoli 1-4, magoli hayo yakifungwa na Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Rafael Daud na Omary Ramadhani, huku mechi ya mzunguko wa pili katika uwanja wa Sokoine kwa mara nyingine tena Mbeya City iliibuka na ushindi mwingine wa magoli 3-1, magoli yaliyowekwa wavuni na Zahoro Pazzi, Tito Okelo na Rafael Daud.

Related news
related/article
Seria A
Giggs: Ronaldo was motivated by Messi
12 Jul 2018, 11:05
FIFA World Cup
Brazil legend: I expected more from Neymar
11 Jul 2018, 18:55
FIFA World Cup
Luka Modric bags the World Cup Golden Ball award
14 hours ago
FIFA World Cup
Pele reacts to Mbappe's success
11 hours ago
Transfer News
Ajax agree deal to sign Manchester United defender
14 Jul 2018, 12:40