Beki wa Zamani wa Tusker FC, achukua tuzo ligi kuu soka Tanzania Bara.

Beki wa Zamani wa Tusker FC, achukua tuzo ligi kuu soka Tanzania Bara.

12 Oct 2017, 16:53

Mchezaji wa timu ya Singida United, Shafik Batambuze amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/2018.

Batambuze anayecheza nafasi ya ulinzi wa pembeni, alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Ibrahim Ajibu wa Yanga na kiungo Mohammed Issa wa Mtibwa Sugar, alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam.

Uchambuzi huo kwa mujibu wa utaratibu hufanywa na kikao cha Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.

Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Singida United kupata pointi 10 katika michezo minne, ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi huo, matokeo ambayo yaliiwezesha Singida United kutoka nafasi ya 10 katika msimamo na kupanda hadi nafasi ya nne kwa mwezi huo wa Septemba.

Msaada wake. 

Singida United ndiyo timu iliyokusanya alama nyingi kwa mwezi huo ukilinganisha na timu nyingine 15 zinazoshiriki VPL.

Singida United iliifunga Mbao FC mabao 2-1 Uwanja wa Jamhuri Dodoma,  ikaifunga Stand United bao 1-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, iliifunga Kagera Sugar Uwanja wa Jamhuri Dodoma na ilitoka sare ya bao 1-1 na Azam FC uwanja huo huo.

Michezo yote hiyo Batambuze alicheza dakika zote 90 kwa kila mchezo, ambayo ni sawa na kucheza dakika 360.

Related news
related/article
Seria A
Modric disappointed by Ronaldo's exit
12 Jul 2018, 18:20
English Premier League
Mahrez appreciates time at Leicester as he begins life at City
11 Jul 2018, 21:45
FIFA World Cup
Drama as pitch invaders interrupt World Cup final
15 hours ago
FIFA World Cup
World Cup Young Player award goes to Mbappe
14 hours ago
Ligue 1
Buffon beaten on PSG debut
19 hours ago