Banda: Tanzania ikifanya hivi itainuka Kisoka.

Banda: Tanzania ikifanya hivi itainuka Kisoka.

05 Oct, 07:09

Mlinzi wa Kimataifa wa Tanzania, anayesakata kabumbu katika Timu ya soka ya Baroka ya nchini Afrika Kusini, Abdi Banda ameeleza kinagaubaga tofauti ya soka la Afrika Kusini na nchini.

Banda ambaye amerejea nchini kwa ajili ya kushiriki mchezo wa Kirafiki wa kimataifa kati ya Taifa Stars na Malawi, amesema kuna mambo mengi ambayo Tanzania wanatakiwa kuyafanya ili kufanikiwa katika soka.

-Ili tuweze kuendelea katika soka kuna mambo mengi, kuanzia viwanja na mambo mengine, kikubwa ni kuamua Tunaanza kitu fulani, lakini kwanza tuanze kuboresha viwanja Inakuwa inavutia hata kuleta wachezaji" Amesema Banda akihojiwa na kipindi cha mshikemshike cha Azam TV.

Maslahi ya wachezaji. 

Banda ambaye amejiunga na Baroka FC akitokea Simba SC amesema jambo lingine ambalo Tanzania wanatakiwa kulifanya ili kukuza soka ni kuthamini wachezaji kwa kuwaboreshea maslahi yao.

-Tuboreshe maslahi ya wachezaji, tuwaheshimu wachezaji, kuna kipindi mpaka ukimwambia mtu unachezea timu kubwa kama Simba SC hawezi kuamini kutokana na maisha yako, watu wanatoka nje Kwa sababu wanataka maslahi mazuri," amesema.

-Nimejifunza vitu vingi, sisi tunafanya Mpira kwenye magazeti Mimi nakuambia Ukweli, kule Mpira kazi" Abdi Banda aliongeza.

Related news
related/article
International News
Germany coach prefers Messi to Ronaldo
26 May, 08:30
Transfer News
Transfer Talk: Midfielder signs permanent deal with Valencia
24 May, 15:20
International News
Andres Iniesta's nine LaLiga triumphs with Barcelona
24 May, 13:05
International News
It's funny if two managers in the final have no clue about tactics - Klopp defends Zidane
25 May, 18:33
International News
MLS Review: LA Galaxy edge San Jose Earthquakes in California Clasico
26 May, 10:31