Mtanzania apata pigo England, kuwa nje ya uwanja miezi mitatu.

Mtanzania apata pigo England, kuwa nje ya uwanja miezi mitatu.

02 Oct, 08:38

Mtanzania Abbas Pira ambaye amejiunga hivi karibuni na timu ya Wrexham FC inayoshiriki ligi daraja la tatu England (National League) amepata pigo baada kuumia akiwa mazoezini.

Pira ameumia kifungo cha mguu baada ya kugongana na mwenzake na kwa mujibu wa Daktari atakaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu na nusu.

-Ni kweli nimepata majeraha, kwenye mazoezi niligongana na striker, baada ya mazoezi nikakutana na specialist akaangalia ankle yangu, na ikaonekana kuna mpasuko kidogo, nimeambiwa nitakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu" Pira ameuambia mtandao huu.

Ni pigo. 

Pira ambaye aliwahi kuitumikia timu ya Coastal Union ya Tanga pamoja na kuwahi kufanya majaribio kunako klabu ya Chelsea ya England amesema anaimani atarejea Disemba mwaka huu.

-Mpaka mwezi wa 12 au wiki ya kwanza ya mwezi wa kwanza mwakani naweza kurudi uwanjani, ni kitu cha kusikitisha kwa sababu ndo kwanza nimejiunga nao," Ameongeza.

Abbas Pira amejiunga na Wrexham FC msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja na bado hajacheza mchezo wowote wa mashindano ama wa ligi, hivyo kuumia kwake kunaweza kuwa ni pigo kwake na kwa Taifa kwa ujumla.

Related news
related/article
International News
Zidane: Madrid not favourites for Champions League final
1 hour ago
Transfer News
Transfer Talk: Villareal midfielder completes move to Atletico Madrid
24 May, 15:50
International News
Iniesta's Vissel Kobe move confirmed
24 May, 11:35
International News
New Arsenal boss Unai Emery's top five past signings
25 May, 09:00
International News
WC 2018: Germany coach defends Ozil,Gundogan
24 May, 15:40